Bwana Abu Talib [a] zimfikie salaamu za Allah (s.w.t). Ninawadondosheeni majauhari yake kutoka Hadith, historia na Vitabu vya sira. Bwana Abu Talib [a] alitunga mashairi katika kumsifu mfalme Najjashi wa Ethiopia ambaye katika mashairi yake anamsifu vile mfalme huyo alivyowapokea, kuwakirimu na kuwanusuru Waislamu ambao walikuwa wamesafiri kutoka Makkah kwenda Uhabeshi. Kama vile anavyotuelezea: (1) Watu wema na wakuu wana elewa kuwa Muhammad ni waziri wa Musa na Masihi Ibun Maryam. Ametujia na mwongozo mfano wa ule walio kuja nao hao wawili, kila mmoja aongoza kwa amri ya Mungu na amenifadhika. Kwa kuwa wao wote wanatuonyesha njia atakavyo Allah (s.w.t). Wao wanafanya uhusiano na watu wote. Na ninyi (Wakristo) mnasoma katika vitabu vyenu kuhusu (Mtume Muhammad [s]) taarifa na sifa zake, hivyo sivyo visa vya uongo, bali ni habari zilizo za kweli. Ewe Najjashi wewe ni mtu mmoja ambaye wakati baadhi ya watu wa Ummah wa Mtume Muhammad [s], wamerudi wakitoa sifa na kukutaarufisha na wala hawakuwa na mambo mengine isipokuwa ukarimu wako.[1] Katika Qasida nyingineyo, Bwana Abu Talib [a] anasema: "Katika kipindi hiki cha ushindi na kunusuru waambie wa Ghalib, Lui na Tiim kuwa (dhidi ya Muhammad) ni harakati zao zisizo na matunda, sisi Bani Hashim ni panga za Mwenyezi Mungu na sisi ndio wenye Ukuu na fadhila juu ya makabila mengine. Je hamujui kuwa kuvunja uhusiano - ni dhambi kubwa sana, kuwa ni upumbavu na ujinga mkubwa sana, je nyie hamuelewi kuwa mwanadamu ataweza kufungukiwa na busara alizojaliwa na Mwenyezi Mungu zilizo dhahiri na batini? Musadanganyike kwa kuona kuwa mna neema za kidunia zitadumu mutambue wazi kuwa hivi si vitu vya kudumu milele bali ni vyenye kuangamia. Isiwe kwamba ndoto hii iwasumbuayo kuwa kumuudhi Mtume Muhammad [s] ukawachukua katika maangamizo na wala isiwe ikawa nyie ndie mukawa ndiyo miguu ya wale Watu wapotofu. Malengo na matakwa yenu yalikuwa ni kwamba huyu Muhammad [s] mumuue, na kwamba ndoto yenu hii imekuwa ikiwasumbua na isiyofua dafu. Nyie mmezani kuwa sisi Bani Hashim tutakupatieni Muhammad [s] na tutakapokuja mbele yenu hatutaweza na wala hatutaweza kumtetea wala kumhami. Mtambueni wazi kuwa huyu ni mmoja wa mitume wa Allah (s.w.t.) ambaye anayeteremshiwa Aya zake Allah (s.w.t.) na yeyote yule atakayemjibu hapana basi huyo mtu daima atakuwa katika majuto na atakuwa akijiuma meno yake. Hebu tazameni mjionee wenyewe, asili na kwa unasaba Hashemi ndiyo wanaomzunguka Muhammad ambao wanawaangaamiza na kuwafukuza wale wote wanaotaka kumdhuru Muhammad.[2] Katika sahifah mojawapo ambayo hapo mbeleni Bwana Abu Talib [a] analielezea shairi lake hivi: "Mimi chochote kile nikisemacho kwa lazima kabila Ia Lui na khususan tawi Ia kabila hili - Bani Kaab! Je nyinyi hamutambui kuwa sisi tunamtukuza Muhammad kama vile alivyokuwa ametukuzwa Musa kwa sababu tunajua kuwa huyu ni Mtume Atakayeteremshiwa kitabu na Aya takatifu za Mwenyezi Mungu na kwamba mapenzi yake yapo katika mioyo ya watu wote. Haijuzu kamwe kumfanyia uadui mtu kama huyu ambaye amechaguliwa kuwa rafiki wa Mwenyezi Mungu. Tahadhari yenu! Tahadhari yenu! Jitahadharini sana musiingie katika makaburi yenu ambamo mutakapoulizwa kuhusu madhambi yenu na mema yenu kwani wakati huo utakuwa ni mgumu mno. Isitokee kwamba ninyi mukausahaulisha ujamaa, udugu na uhusiano wetu bora uliokuwapo na mukaingia kwa kutumbukia katika mashimo ya wale walioasi na madhalimu. Basi mimi kwa kula kiapo cha nyumba ya Mwenyezi Mungu ninasema kuwa sisi kamwe hatutamsalimisha Muhammad mbele ya maadui wake hata kama itatubidi sisi tukabiliane na kupambana na vile vile tustahimili magumu na misiba ya kila aina. Je sisi si watoto wa Hashim ambaye daima alikuwa akitupatia silaha na kututayarisha kwa ajili ya vita na kuwausia watoto wake daima wawe washupavu na hodari? Na hii ndiyo sababu moja kubwa kabisa kamwe hatujahisi na wala hatuhisi na hatutahisi magumu ya vita na kwa sababu hiyo kubwa sisi kamwe hatutarudi nyuma kutokea uwanja wa vita. Sisi daima tuko imara na thabiti katika shida na misiba yote na wala kamwe hatupigi makelele badala yake sisi tunakuwa tukijiimarisha na kuwa madhubuti zaidi katika vita vyetu ambavyo hata mahodari katika nyanja hizi nao wanashindwa na kufa nguvu.[3] Katika baadhi ya mashairi yake yapo yafuatayo: Ni jambo la kusikitisha kuwa nyota ya mwisho wa usiku imenitia katika mabano ya huzuni, ingawaje nyota ya matumaini bado haijazama. Nyota hii ya huzuni imenishtua wakati macho mengi yalikuwa yamefungwa na wale waliokuwa macho wamekuwa mashughuli katika kuhadithiana visa. Kisa hiki kinaelezea ndoto zile za kuteseka cha wale ambao wanataka kumghilibu Muhammad, ili waweze kumfanyia dhuluma. Lakini mtu ambaye hawezi kujimudu kwa kuzidi kwake basi mtu huyu mwenyewe anatumbukia katika dhuluma mojawapo. Wao kwa hasira na juhudi zao na kwa matendo yao maovu wameanza kuongozwa na hizi ndoto mbaya zenye kuangamiza na kuleta majuto hapo mbeleni. Wao wanategemea kuwa sisi tutafanya kazi moja kubwa - yaani tutamsalimisha Muhammad mikononi mwao, ingawaje kazi hii haitawezekana kamwe bila ya kutumika kwa mapanga, mishale na mikuki yaani bila kutokea kwa vita, haiwezekani. Wao wanadhani kuwa sisi bila ya kutumia mapanga yetu katika vita tutakubali kumsalimisha Mtume Muhammad [s] ili mapanga yao yajae damu huku sisi tukiwia radhi. Basi wale Bani Fahr wakae kwa tahadhari bado hawajazisikia sauti zao kuuliwa ambayo yatakuwa yamejaa kwa masikitiko na masiba na shida mbali mbali. Fikirieni vyema kabisa kuwa mazungumzo yetu haya ni yenye faida kubwa kwa upande wenu na wala isije ikatokea kuwa nasaha zetu hizi zikipuuzwa zikafungua milango ya vita moja kwa moja.[4] Katika shairi mojawapo akiongea na Mtume Muhammad [s], Bwana Abu Talib [a] anasema: "Kwa kiapo cha Allah (s.w.t)! Kutokana na wingi wa majeshi yenu na nguvu zenu, kamwe kamwe hamutaweza kutughilibu. Hivyo munaweza kuvitumikia tu hadi pale vinapokuwa na roho kabla ya kuuawa. Kwa hivyo ni nasaha zangu kuwa (Ewe Mtume Muhammad [s]) tangaza Da'awa yako dhahiri kwa sababu humo hakuna jambo la aibu wala upotofu. Notes: [1] Mustadrak Hakim, J. 2, uk. 623 kwa kutokea Ibn Is-haq [2] Ibn Abi Hadid, Juz. 3, Uk. 313 [3] Sirah Ibn Hisham, J. 1, UK. 373; Sharh Nahjul Balagha Ibn Abi al-Hadid, J. 3, uk. 313; Bulugh-al-Arab, J. 1, uk. 325; Khazana-al-adab li-Baghdadi, J. 1, uk. 261; Rawdh-al Anaf, J. 1, uk. 220; Tarikh lbn Kathiir, J. 3, uk. 87; Isni al-Matalib, uk. 6-13; Talabat al-Talib, uk. 10 [4] Sharh Najul Balagha, lbn Abi Al-Hadid, J. 3, uk. 3312.
|