Salaam zimfikie kiongozi wa Makkah Bwana Abu Talib [a] kwa sababu yeye amemsaidia Mtume Muhammad [s] kwa kila hali kwa kumhifadhi na vile vile kwa jitihada zake katika kuinusuru dini ya Islam na kuyaweka maisha na kwa kuwaita na kuwalingania katika dini ya Islam katika hali ya hatari na misukosuko mbalimbali kuanzia pale Mtume Muhammad [s] alipoutangaza utume wake na kwa jitihada zote na harakati zote tunazozijua na zote zile tutakazozisoma humu kitabuni na kusikia kutoka kwa wanazuoni wengine zinatuthibitishia wazi kuwa yeye alikuwa ni Mwislamu halisi na mwenye imani kamili na alikuwa ni mtu ambaye anayo imani kamili juu ya Mtume Muhammad [s] ndivyo yanavyodhihirisha matendo na jitihada zake. Kwa imani yake hii kwa Allah (s.w.t.) na utiifu wake kwa Mtume Muhammad [s] Inshaalah itakuwa dhahiri na bayana siku ya Qiyamah, hata hivyo sisi hapa tunajaribu kwa mukhtasari na uwezo wetu mdogo kuwaleteeni machache kuhusu vile alivyokuwa ameisimamia dini ya Islam kwa ushupavu na umadhubuti na jitihada zake zote katika kuinusuru na kuieneleza dini ya Islam kwa hali na mali.
|