lbn Is-haq anasema: Bwana Abu Talib [a] alikuwa akienda pamoja na msafara wa wafanya biashara kuelekea Sham (Syria). Wafanya biashara hao walijitayarisha wakiwa na shehena yao ya lazima na walijiandaa kuondoka na mara akatokea Mtume Muhammad [s] na akashika hatamu (kamba) ya ngamia na akasema: "Ewe Baba yangu! Je mimi unaniacha mikononi mwa nani, ukiondoka? Wakati unatambua kuwa mimi sina baba ambaye atanisaidia na wala sina mama atakayenipa mapenzi yake?" Kwa kusikia haya Bwana Abu Talib [a] alipitiwa na hali tofauti, na baada ya kujimudu akasema: "Kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu! Mimi nitamchukua huyu pia kwa sababu siwezi kamwe kutengana naye na wala yeye kamwe hawezi kutengana nami! Hivyo Mtume Muhammad [s] akaweza kwenda pamoja na msafara wa Bwana Abu Talib [a] kuelekea Sham. Pole pole msafara huo ulielekea na kufika katika mji wa Basra ambao ulikuwa chini ya himaya ya Sham. Njiani humo msafara ukipitia katika kanisa moja ambamo kulikuwa na Padri mmoja akiitwa Buhaira ambaye alikuwa mwenye ilimu sana na alikuwa akiwahudumia wasafiri wa Kikristo huko. Naye alikuwa akiwapatia Wakristo ilimu ya dini yao kutoka katika kitabu alichokuwa amekipata katika urithi wake. Ingawaje misafara mingi kama hiyo ilikuwa imekwishampitia huyo Buhaira, yeye kamwe hakuizingatia misafara hiyo wala hakuwa akizungumza nao hadi ulipofika mwaka huo wakati msafara huo kutoka Makkah ulipofika hapo karibu naye. Msafara huo ulipokaribia na Kanisa hilo, waliweza kufunga mahema yao na kufanya kituo hicho chao cha mapumziko. Kwa sababu hii imetokana na yeye kuona kutokea katika kanisa lake nuru iliyokuwa ikiteremka kutoka mbinguni ikiwa katika sura ya wingu ambalo lilikuwa likienda pamoja na msafara huo kwa sababu alikuwamo mtu katika msafara huo akikingwa na miale ya jua hata pale msafara huo ulipokuwa umepumzika chini ya mti. Na aliweza kuona vile vile matawi ya mti huo yakiinama kutoa heshima. Na mtu huyo alikuwa ndiye Mtume Muhammad [s]. Buhaira aliyaona hayo yote na kutoka nje ya kanisa na kuwaamrisha watu wake waanze kufanya matayarisho kwa ajili ya kuwakirimu wasafiri hao na wakati vyakula vilipokuwa tayari aliwatumia ujumbe ufuatao: "Enyi kundi la Maqureishi! Mimi nimewatayarishieni vyakula na ninataka ninyi nyote wakubwa kwa wadogo, watumwa na wote walio huru - mje katika karamu yangu hii." Mtu mmoja kutoka msafara huo akaenda kumwuliza Buhaira ni hoja gani iliyomfanya yeye kuwakirimu leo kwani daima wamekuwa wakipita hapo bila hata ya kuwajali! Buhaira alijibu: "Ndiyo! leo nimeona dalili tofauti kabisa na kwa sababu hiyo mimi niwe mkirimu wenu usiku huu mtakapokuwa katika kituo chenu hicho. Mimi nimewatayarishieni vyakula ili mje mle na kupumzika vyema katika kituo hiki karibu yetu." Hivyo watu wote waliokuwa katika msafara huo walikwenda kwake isipokuwa Mtume Muhammad [s] kwa sababu ya udogo wa umri wake, walimwacha kituoni humo akiwa pamoja na mizigo ya wasafiri. Buhaira alipowatupia macho yake hakuona ishara yoyote ile makhususi na hivyo aliwauliza iwapo kuna mtu yeyote kati yao ambaye hajafika hapo. Wao walimjibu: "Wale wote waliokuwa, wakistahiki kuja wamefika hapa isipokuwa yupo kijana mmoja ambaye ana umri mdogo.. tumemwacha kituoni pamoja na mizigo yetu." Buhaira akawaambia: "Haiwezekani kumwacha mtu yeyote ila aje ashiriki pamoja nasi katika karamu hii." Mmoja miongoni mwa Maqureishi akasema: "Kwa kiapo cha Lat na Uzza[5]! Leo lazima kunajambo la ajabu!" Je sasa hi kweli itawezekana kwetu sisi kumtenga Mtume Muhammad [s] kwa kutoshiriki katika karamu hii na mara akainuka na kaenda kwa Mtume Muhammed [s] akambeba na kumleta miongoni mwao ili ashiriki katika karamu hiyo. Buhaira alipomtupia tu jicho kijana huyo alishangaa kwa sababu ubashiri na dalili zote alizokuwa akizijua za kuja kwa Mtume aliziona katika kijana huyo (Mtume Muhammad [s]) na hivyo alikuwa akijaribu kuzipeleleza na kujaribu kuthibitisha kwa kila ubashiri na dalili alizokuwa akizijua. Wakati huu wasafiri wote walikuwa wamekwisha kula na kurejea katika kituo chao kwa mapumziko. Buheira aliinuka na kumwendea Mtume Muhammad [s] na akamwambia: "Ewe mwana! Kwa kiapo cha Lat na Uzza' kuwa kile nitakachokuuliza utanijibu kwa usahihi". Mtume Muhammad [s] alimwambia: "Kamwe usiniulize kwa viapo vya Lat na Uzza'. Buhaira akasema: "Vyema basi ninakupa viapo vya Mwenyezi Mungu." Hapo ndipo Mtume Muhammad [s] alisema: "Tafadhali uliza kile utakacho." Hapo Buhaira alianza kumwuliza mambo mengi ambayo alikuwa ameyasikia na kuyajua kuhusu mambo yatakayotokea hapo siku za usoni. Ndipo Mtume Muhammad [s] alipoendelea na hoja zake alizoziuliza. Majibu ya Mtume Muhammad [s] yalikuwa kwa mujibu wa dalili alizokuwa akizijua Buhaira kuhusu Mtume atakayekuja. Baadaye Buhaira alilitazama bega la Mtume Muhammad [s] kama vile alivyokuwa akijua yeye na akauona muhuri wa Utume. Kwa tukio hili Bwana Abu Talib [a] amelizungumzia hivi katika mashairi yake. Kwa hakika mwana wa Amina, Mtume Muhammad [s] katika macho yangu anao daraja kubwa sana hata kuliko watoto wangu! Na wakati ngamia wangu walipokuwa wakiondoka kwa safari yeye aliwashika hatamu na hapo uadilifu wangu ukajaa vile alivyokuwa yeye mwenye kuwasaidia na kuwanusuru wengi mno na mimi nilipomwita aje miongoni mwa watu atembee na azunguke wakati msafara wa kwenda mbali ulipokuwa tayari kwenda mbali. Hapo mji wake ameuacha mbali mno kiasi kwamba wakajikuta wamefika Basra. Huko yeye akakutana na Padri Buhaira aliyekuwa akimsubiri kwa hamu ya muda mrefu. Yeye alimwelezea kuhusu Mtume Muhammad [s] dalili za kweli na aliomba wale wote wenye husuda wasimkaribie kamwe. Wakati kikundi kimoja cha Mayahudi walipoona kuwa Mtume Muhammad [s] alipokuwa akienda kulikuwa na wingu likimfuata juu yake basi wakakutana na kuafikiana kuwa wamuuwe Mtuume Muhammad [s]. Lakini Buhaira alijitolea kifua wazi na aliweza kuwazuia Mayahudi hao wasiweze kumuuwa Mtume Muhammad [s]. Na kwa ajili ya suala hili Bwana Abu Talib [a] amesema mashairi yafuatayo: Je mimi nilipokuwa nimenuia moyoni mwangu kuhusu safari yangu ya kuelekea Sham, je wewe hukuiona hali yangu ilivyokuwa? Kwa hakika safari hii ilikuwa ya lazima kutengana, utengano ambao wazazi wanavyouhisi ulivyo mgumu utengano huo ulikuwa na Mtume Muhammad [s] wakati ambao mimi nilikuwa nimejitayarisha kwenda Sham. Lakini nilijikaza na kuondoka na kumtakia kila la kheri hadi nitakaporejea na yeye kwa huzuni na hofu alikuwa akilia na ngamia walikuwa baina yetu wawili. Na Mtume Muhammad [s] ndiye aliyekuwa ameshika kamba ya ngamia. Mimi nilimkumbuka sana baba yake na niliangua kilio kwani daima nilikuwa nikimlilia. Bwana Abu Talib [a] aliendelea kuelezea kuwa mimi nilimruhusu Mtume Muhammad [s] aje pamoja nasi katika msafara huu." Bwana Abu Talib [a] anaongezea katika mashairi yake hivi. Sisi tulipewa makaribisho mazuri sana na huduma nzuri kabisa hapo Basra na tulijiwa na Buhaira ambaye alitupatia kila aina ya huduma na alituambia kuwa tuwalete watu wetu wote katika karamu aliyokuwa ametuandalia bila ya kukosa hata mmoja wetu. Sisi tulimwambia kuwa sisi sote watu wazima tulikuwa tumefika isipokuwa kijana mmoja mdogo ndiye tuliyekuwa tumemwacha hapo nyuma ambaye ni yatima pia. Lakini Buhaira alimwita kijana huyo mdogo. Alituambia kuwa kulikuwapo na vyakula vingi mno hivyo haikuwapasa kumwacha nyuma kijana huyo na kama wasingemleta huyo kijana mbele yake kushiriki katika karamu hiyo hasi asingewaheshimu kamwe. Na Buhaira alipomwona Mtume Muhammad [s] akija kuelekea nyumba yake huku akiwa amefuatwa na wingu juu yake, hapo ndipo Buhaira alipojitupa chini huku akisujudu na kwa mapenzi mno alimkumbatia Mtume Muhammad [s][6] [5] Lat na Uzza' ni majina ya miungu iliyokuwa ikiabudiwa kabla ya kuja kwa Uslamu. [6] Diwan Abu Talib [a], J. 4, uk. 33-35; Tarikh Ibn Asakir, J. 1, uk. 269-272; Riwdha-al-Anaf, J.1, uk. 120.
|