Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
BWANA ABU TALIB [A] AOMBA MVUA KWA WASILA WA MTUME [S]

Jalhama ibn Urfatah anasema: Wakati mmoja mimi nilifika Makkah ambapo wakazi wake walikuwa katika mpito wa kipindi shadidi cha ukame na njaa kali.

Maquraish wakasema: "Ewe Abu Talib chemchemi zote zimekauka na wakazi wote wa mji wameathirika mno kwa ukame pamoja na njaa hii kali. Hivyo twendeni sote tukusanyike ili tuombe kwa Mwenyezi Mungu atuondolee balaa hii kubwa iliyotukumba.

Hapo tukamwoona Bwana Abu Talib [a] anatoka nje huku akiwa amemshika mkono kijana mmoj, mtoto huyo ni Mtume Muhammad [s] aliyeonekana akiwa kama jua ilivyo nyuma ya wingu jeusi. Pamoja na Mtume Muhammad [s] kulikuwapo na watoto wengi. Bwana Abu Talib [a] alimwinua Mtume Muhammad [s] juu na kumwegemesha juu ya kuta za Al-Kaaba na wakati bado huyo kijana akiwa yungali katika mikono ya Bwana Abu Talib [a], aliomba dua ya kupata mvua.

Ingawaje wakati huo kulikuwa hakuna mawingu ya mvua hapo angani ikaonekana kuwa mawingu yameanza kukusanyika kutoka sehemu mbalimbali na muda si mrefu mvua ilianza kunyesha mito, mabwawa, mashamba na makonde yote yalijaa maji kwa kiasi kilichohitajika na hivyo maisha neema yakarudia kama kawaida. Kwa tukio hili Bwana Abu Talib[a] aliyasema mashairi yafuatayo:

Mtume Muhammad [s] ni mtukufu kiasi kwamba mawingu yanapoona uso wake yanajawa kwa maji ya kunyesha mvua yeye huyu, yatima atawanusuru mayatima na atakuwa mlezi wa wajane na wanaukoo wa Hashim ambao wanakuwa na misiba na shida basi watakuwa wakisaidiwa na wakifarijiwa na huyu. Nao wataishi maisha ya neema. Huyu Mtume Muhammad [s] ni mizini ya uadilifu kwamba hatadhulumiwa mtu yeyote hata kwa kiasi cha punje ndogo

Huyu atakuwa na ilimu na maarifa kiasi kwamba watu hawatakuwa na uwezo wa kupima ilimu na fahamu zake.[7]

Mambo haya yanadhihiri wazi kabisa kuwa Bwana Abu Talib [a] alikuwa akielewa vyema kabisa wadhifa na daraja Mtume Muhammad [s] na utume wake na alikuwa na imani kamili juu ya maswala haya. Tumeona tukio moja muhimu kabisa kuwa huko Makkah kulikuwa na ukame na njaa ya hatari kabisa kwa hivyo kulipopita kipindi cha miaka miwili mfululizo bila ya kunyesha mvua basi Bwana Abdul Muttalib alimwamrisha mtoto wake Bwana Abu Talib [a] kuwa amchukue Mtume Muhammad [s] na kumviringisha katika nguo kwani wakati huo Mtume Muhammad [s] alikuwa yungali mtoto mchanga kabisa na baadaye Bwana Abdul Muttalib alielekea al-Kaaba tukufu na alimwinua juu Mtume Muhammad [s] huku akisema:

"Ewe Mwenyezi Mungu! Kwa ajili ya mtoto huyu aliye mkononi mwangu (na alirejea senteso hii kwa mara tatu na akaendelea kusema) "Ewe mwenyezi Mungu! Kwa ajili ya mtoto huyu tunaomba utunyeshee mvua moja kwa moja. Na kulikuwa hakujapita muda watu wakaanza kuona mawingu ya kunyesha mvua ambayo ilinyesha kwa wingi kiasi kwamba watu walianza kuingiwa na hofu ya kuporomoka kwa Masjid al-Haram kwa mafuriko.[8]

Wakati huo Bwana Abu Talib [a] alisoma Qasida hii.

Mtume Muhammad [s] ni mtukufu kiasi kwamba mawingu yanapoona uso wake yanajawa kwa maji ya kunyesha mvua yeye huyu, yatima atawanusuru mayatima na atakuwa mlezi wa wajane.

Hivyo Bwana Abdul Muttalib kwa kuomba dua ya mvua kumwomba Mwenyezi Mungu kwa wasila wa Mtume Muhammad [s] na vile vile Bwana Abu Talib [a] naye pia kuomba mvua kwa wasila wa Mtume Muhammad [s] wakati mtume akiwa bado kijana. Hivyo matukio haya mawili yanatuthibitishia kuwa wazee hawa wawili walikuwa wakijua utukufu na kuwa Mtume Muhammad [s] ataleta dini ya haki yenye kuwaita watu katika kumuabudu mmoja tu hivyo wao walikuwa na imani kamili juu ya Mtume Muhammad [s].

Hivyo matukio haya mawili ya kihistoria yanaonyesha waziwazi vile yakithibitsha imani zao kamili juu ya Tawhidi na Utume. Hivyo vinatutosheleza sisi matukio haya mawili kuona na kuamini, wazee hawa wawili Bwana Abdul Muttalib na Bwana Abu Talib [a] walivyokuwa na imani kamili juu ya Tawhid, Utume, na Mtume Muhammad [s].

 

[7] Qastalani, Sharh Bukhari, j. 2, uk. 327; Mawahib li-diniyya, j. 1, uk. 48; Khasais al-Kubra, j. 1, uk. 86-124; Sharh Bihujjatil mahafil, j.1, uk. 119; Siira Halabiyyah, j. 1, uk. 125; Wahlan, Surat an- Nabawiyyah, j. 1, uk. 87; Talabat al-Talib, uk. 42; Taarikh ibn Asakir.

[8] Shahristani, Milal wa Nihal, maelezo sura ya 3, uk. 225