Jaabir ibn Abdullah anasema: Mimi nilimwuliza Mtume Muhammad [s] kuhusu kuzaliwa kwa Imam Ali [a] na Mtume Muhammad [s] aliniambia: "Bila shaka, ewe Jaabir! umeniuliza kuhusu yule anayezaliwa ambaye ni mtu bora kabisa ambaye ni sawa na Masihi ibn Maryam. Allah (s.w.t.) ameniumba mimi na Ali [a] kwa nuru moja i.e. mimi kwa nuru ya Ali na Ali kwa nuru yangu. Na sote tulikuwa pamoja hadi ukafika wakati mimi nikapitia tumbo Ia mama yangu Amina na Ali [a] akapitia katika tumbo la mama yake Fatema binti Asad ndio kuzaliwa kwake. Katika zama zile kulikuwa na Mubiram bin Daayab bin Ishkebani ambaye alikuwa ni mcha mungu mmoja ambaye kwa muda wa miaka mia mbili na sabini alikuwa akifanya ibada ya Mwenyezi Mungu tu bila hata ya siku moja kumwomba mola wake ombi lolote. Ikatokea kwamba Allah (s.w.t) akamtuma Bwana Abu Talib [a] aende kwa huyo mcha mungu. Mcha mungu huyo alipomwona Bwana Abu Talib [a] amemjia basi akainuka kutoka nafasini mwake na akaubusu uso wake na kumkalisha karibu nae. Hapo ndipo alipomwuliza Bwana Abu Talib [a] kuwa yeye ni nani?" Bwana Abu Talib [a] akajibu: "Mimi ninao uhusiano na Tahama". Mcha mungu huyo alimwuliza "Tahama anatokana na kabila gani?" Bwana Abu Talib [a] akamjibu: "Mimi ninatokana na ukoo wa Bani Hashim." Kwa kuyasikia hayo, mchamungu huyo aliinuka kutoka nafasini mwake na kwa mora nyingine tena aliubusu uso wake na akasema: "Ewe Bwana! Mwenyezi Mungu amenibashiria habari Fulani." Hapo Bwana Abu Talib [a] kwa shauku ya kutaka kujua akamwambia "Je ubashiri huo ni upi, naomba uniambie." Mchamungu huyo alianza kumwambia: "Katika kizazi chako atazaliwa mtoto mmoja ambaye atakuwa ndiye walii wa Mwenyezi Mungu Wakati ulipofika usiku wa kuzaliwa kwa Imam Ali [a] usiku huo ulikuwa wa kung'ara mno, basi Bwana Abu Talib [a] alionekana akitoka nje huku akisema kwa furaha mno kuwa amezaliwa walii wa Mwenyezi Mungu katika al-Kaaba tukufu. Usiku huo ukapita na siku ya pili ikafuata mnamo wakati wa mchana Bwana Abu Talib [a] alingia katika al-Kaaba tukufu huku akiyasema mashairi yafuatayo: "Ewe Mola kiangamize kiza hiki, Ewe Mola wa kuleta nuru ya mwezi tunaomba utudhihirishie amri yako iwe dhahiri kwetu. Tunaomba ubashiri wako katika kumpatia jina huyu mtoto. Baada ya hapo Mtume Muhammad [s] akasema: "Wakati huo nikasikia sauti moja kutoka mbinguni ikisema: "Enyi watu wa ukoo wa Mtume Muhammad [s] mpenzi mmebahatiwa kumpata mtoto mpenzi na mtoharifu, jina lake kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni Ali ambalo limetokana na jina lake Mwenyezi Mungu la A'ala.[9] [9] Kanji Sahafi, Kifayat al-Talib, uk. 260
|