 |
KUPOTEA KWA MTUME MUHAMMAD [s]
Maquraish wote walikusanyika katika ijitimai, mkutano mkubwa huko nyumbani kwa Bwana Abu Talib [a] kuhusu da'awa ya Mtume Muhammad [s]. Wao wote kwa pamoja walianza kudhihirisha chuki, hasira na vitisho vya dhidi ya Mtume Muhammad [s]. Waliinuka kwa hasira na ghadhabu na walijawa na mawazo ya kulipiza kisasi; "Sasa sisi sote kwa pamoja tuinuke kutoka hapa na tuondoke zetu na tuendelee kuabudu miungu yetu kama vile tulivyokuwa tukiabudu hapo awali. Bila shaka katika tablighi hii kuna maslahi yao." [11]
[11] Al-Qur'an, Sura Saad Aya 6
|