Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
UTANGULIZI

Maisha ya mwanadamu ni mnyororo wa mapambano. Ni lazima apambane katika kuyashinda mapenzi yake na misukumo ambayo ni lazima imkabili kwa vile yu mwanadamu, naye ni lazima kuwa macho katika unyonge wake na kuyatii maamrisho yote ya akili zake kuhusu mambo yote anayoamini kuwa ni bora zaidi kuliko aina zote za starehe. Na kwa upande mwingine ni lazima ajiambatanishe na njia yake ya ukweli katika meno ya nguvu zote zinazompinga ambazo humkingia njia yake. Hana budi kupigana na dhoruba ya fikara, mapokeo, faida za daima na zile nguvu zote za dhuluma na uovu ambazo humfikiria mtu huyu kuwa yu mwovu, na hivyo kumfanyia chanzo cha kuyarudisha nyuma maendeleo yake.

Vitabu vya akhlaki (elimu ya tabia nzuri au mema na mabaya vimejaa mafundisho ya kale, lakini tunahitaji kuona mifano ya siku hizi ya kutushawishi, kuifuata mifano hiyo. Imamu Husayn [a] alikuwa mfano wa aina hiyo.