Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
KUFARIKI KWA MTUME [s]

Alipofariki Mtume [s] Imamu Husayn [a] alikuwa na umri wa miaka sita tu. Kipindi cha miaka ishirini na mitano kilichofuatia ambacho Imamu Ali [a] aliishi maisha ya kujitenga, Imamu Husayn [a] alipata muda wa kutosha kujifunza tabia za babiye. Mafunzo haya yalichukua muda wa ujana wake na alipokuwa na umri wa miaka thelathini na moja baba yake alipewa Ukhalifa. Imamu Hasan [a] alifuatana na babiye katika vita za Jamal, Siffin na Nahrawan. Katika mwaka wa 40 Hijiriya Hadhrat Ali [a] alikufa kishahidi katika msikiti wa Kufa (Iraq) na Imamu Hasan [a] alilazimika kuzishika kazi za Ukhalifa. Imamu [a] Husayn akiwa ndugu mtiifu, alimsaidia Imamu Hasan [a] na Imamu Hasan [a] alipofanya mapatano na Muawiyyah ili kuziokoa haki za Uislamu, Imamu Husayn [a] nae aliishi maisha ya kujitenga kama alivyofanya Imamu Hasan [a]. Imamu Husayn [a] alitumikia Uislamu kimya kimya kwa muda wa miaka ishirinl. Miaka kumi chini ya kaka yake Imamu Hasan [a] na miaka kumi baada ya kifo cha Imamu Hasan [a]. Lakini katu Muawiyyah hakuyatimiza masharti ya mapatano aliyoyafanya na Imamu Hasan [a]. Alimtilia sumu Imamu Hasan [a] na akawasumbua sana wafuasl wa Imamu Ali [a] na akawafunga, akawakata vichwa na hata kuwasulubisha. Mwishoni kabisa alivunja masharti ya mapatano kwa kumchagua mwanawe Yazid kuwa mrithi wake na alitumia kila aina ya nguvu na propaganda ili kuungwa mkono wa Waislamu.