Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
TABIA YAKE

Imamu Husayn alikuwa lmamu wa tatu na alikuwa mcha Mungu na mnyofu sana. Hata maadui wake waliukubali ukarimu wake na sifa zake nzuri. Alikuwa akienda Sajdah elfu moja katika muda wa masaa ishirini na manne (siku moja). Alikwenda Hija mara ishirInI na tano kwa miguu. Mtukufu Mtume [s] yeye mwenyewe alisema, "Husayn ana ushupavu na ukarimu wangu". Mlangoni pake kila wakati palikuwa na maskani na kila mara nyumba yake ilijaa wageni na hakuna mtu yeyote yule aliyerudi kutoka nyumbani kwa Imamu Husayn [a] bila ya kuridhika. Kwa sababu hiyo alikuwa akijulikana kwa jina la "Baba wa maskini". Alikuwa na kawaida ya kuchukua mikungu ya tende na mikate wakati wa usiku kwenda kuwapa watu fukara na maskani. Na kazi hizi za usiku ziliweka alama katika mgongo wake. Kila mara alikuwa akisema, "Kama akikujia maskini yeyote yule kutaka msaada, ina maana kuwa maskini huyo kakuuzia heshima yake na sasa ni wajibu wako kutomrudishia akiwa na wazo baya kuhusu heshima yako."

Jinsi alivyokuwa akiwatendea watumwa na watumishi wake ilikuwa na kama vile atendavyo baba mwenye huruma. Kila mara alikuwa akitafuta nafasi ya kuwapatia uhuru.

Watu wote wa wakati wake waliitambua vizuri elimu yake bora. Katika kila tatizo Ia kidini aliendewa na kutakiwa alitatue tatizo hilo. Mkusanyo wa Sala zake unaoitwa "Sahifah Husayniah" (kitabu cha Husayn) upo hadi sasa.

Ailkuwa na huruma sana kiasi ambacho aliwaonea huruma hata maadui zake. Kila mara aliwashughulikia sana maskini wa watu wengine kabla ya wale maskini wake. Imamu Husayn [a] akiwa na sifa zote hizi nzuri. Alikuwa mpole na mnyenyekevu sana kiasi ambacho siku moja alipokuwa akipita mahali Fulani maskini fulani walimkaribisha kula chakula pamoja nao. Imamu [a] alikwenda kukaa pamoja nao ingawa hakuweza kula nao kwa kuwa sio halali kwa watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume [s] kutumia chochote kile kilichotolewa sadaka.

Matokeo yake yalikuwa kila awapo, watu hawakuweza kumtazama. Aliheshimiwa sana kiasi ambacho hakuna mtu ye yote yule aliyezikataa sifa zake nzuri, hata wale wa kabila lililokuwa adui kwa ukoo wake. Siku moja alimwandikia barua kali sana Muawiyyah akimlaumu kwa matendo yake yasiyo sahihi. Muawiyyah alipoisoma barua hiyo alichomwa sana moyoni. Wafuasi wake walimshauri amwandikie Imamu [a] barua kama hiyo. Muawiyyah alijibu, "Kama nikiandika mambo yasiyo ya kweli katika barua hiyo basi barua hiyo haitatimiza lengo lake, na kama nikijaribu kutafuta upungufu wowote ule katika tabia zake (lmamu Husayn [a]), Wallah, nashindwa kupata wowote ule".

Masaibu ya Karbala wanaonyesha sura ya ushujaa wake, ukweli, nia, uvumiIivu, ustahimilivu na amani. Hakuzilegeza juhudi zake katika kufanya mapatano hadi mwisho, lakini hakukubali kugeuka japo inchi moja kutoka kwenye njia yake ya wajibu wake na aliridhika kufa kuliko kufanya hivyo.

Aliishi akiwa mwana chini ya baba yake Imamu Ali [a] na akiwa ndugu mdogo wa Imamu Hasan [a] na aliwatii kwa kuwa ilikuwa haki kwake kufanya hivyo. Huko Karbala aliwaongoza watu wake vizuri sana kama alivyowatii wakubwa wake. Imamu Husayn [a] yu mnara wa taa ya Uongozi kwa wanadamu wote.