Moja ya masharti muhimu sana ya mapatano yaliyofanywa baina ya Imamu Hasan [a] na Muawiyyah ni kuwa Muawiyyah hana haki ya kumchagua mrithi wa Ufalme wake. Lakini kama alivyovunja masharti mengine ya mapatano hayo, vile vile alilivunja sharti hili nalo bila ya aibu yoyote ile. Sio kuwa tu alimchagua mwanawe Yazid kuwa mrithi wa Ufalme wake, bali vile vile alifanya msafara wa kuwatembeIea Waislamu na kuwataka wafanye "Baiat" (kiapo cha utii) kwa ajili ya mwanawe. Imamu Husayn [a] alikataa jambo hilo. Sio kuwa tu Yazid hakuwa na haki ya kuwa Khalifa, lakini kama kila mmoja wetu ajuavyo sana siku hizi, alikuwa na tabia mbaya sana kiasi ambacho hata kuzitaja tu tabia zake ni uchafu mkubwa. Na vivyo katika hali hiyo Muawiyyah alitaka kibali cha kuidhinishwa kwa tabia hizo mbaya za mwanawe kwa kibali cha lmamu Husayn [a] cha kuteu1iwa kwake kuwa Khalilfa. Hivyo baada ya kifo cha Muawiyyah, jambo Ia kwanza alilolifanya Yazid lilikuwa ni kujaribu kupata kibali cha Ukhalifa wake kutoka kwa Imamu [a]. Hivyo, alipomwandikia gavana wa Madina kumjulisha kifo cha baba yake, Muawiyyah, vile vile alimwandikia kuhusu jambo hilo. Gavana huyo aliyeitwa Walid alimwita Imamu Husayn [a] na kumweleza ujumbe wa Yazid. Kukubali au kupatana na Imamu [a] kuhusu jambo hili hakukuwa kitu cha kutegemea. Imamu [a] alijua vizuri sana kuwa haiwezekani kwake kuukubali utawala wa Yazid; na vile vile pia alijua matokeo yatakayotokana na kukataa kwake. Lakini njia ya wajibu wake ilikuwa wazi kabisa kwake. Hivyo baada ya kumpa Walid jibu Iifaalo, Imamu [a] alirudi nyumbani. Baada ya Imamu [a] kuona kuwa haingefaa kwa yeye kuendelea kukaa Madina, aliamua kuondoka mjini humo. Siku hiyo alipoondoka Madina ilikuwa ni tarehe 28 ya mwezi wa Rajab mwaka wa 60 Hijiriya. Kwa vile mji wa Makka ulikuwa mahali pa kukimbilia kwa watu wote kufuatana na desturi za watu wa Uarabuni na sheria za Uislamu kwa ujumla, Imamu [a] pia alikwenda huku. Aiifuatana na jamii yake wakiwemo wanawake wa ukoo wa Mtukufu Mtume [s] na hata watoto. Wakati huo, wakati wa Hija ulikuwa karibuni sana na Imamu [a] alitaka kuhiji. Lakini Imamu huyu aliyekwenda kuhiji huko Makka mara ishirini na tano kwa miguu, safari hii alilazimika kuondoka mjini humo bila ya kuhiji. Serikali shari ya Shamu ilituma watu kadhaa kwa jina Ia mahujaju ili kumuulia mbali lmamu [a], hata kama wakiifanya dhambi hii ndani ya Kaaba yenyewe, si kitu. Imamu [a] hakupenda kuona utakatifu wa Kaaba ukivunjwa kwa sababu yake. Siku mbili zilipobakia kwa Hija, lmamu [a] aliondoka Makka pamoja na jamii yake yote na wafuasi wake. Kwa kuwa alikuwa akipokea barua kutoka Kufa, zikimtaka aende huko na zikisisitiza kuhusu kumkubali kuwa yu Imamu wa haki, Husayn [a] katika hali hii ya kutoweza kuamua, alianza safari yake kwenda Iraq. Alimtuma binamu yake Bwana Muslim bin Aqil kwenda Kufa kutazama hali ilivyo na kumjulisha Imamu [a]. Bwana Muslim alipofika Kufa alipokewa vizuri sana lakini upesi sana Yazid alimteua Ubaidullah Ibn Ziyad kuwa gavana wa Kufa na mtu huyu aliyekuwa katili sana miongoni mwa watu wa kabila ya Bani Umayyah, mara moja alitoa amri kali sana kuhusu Bwana Muslim bin Aqil. Akaufunga mji wote na mara moja wale wote waliokuja kuonana na Bwana Muslim waliondoka mjini humo. Mnamo tarehe 9 ya mwezi wa Dhul Hajj (Mfunguo Tatu) mwaka wa 60 wa Hijiriya Bwana Muslim bin Aqil alikamatwa na akauwawa kikatili sana. Habari za kuuwawa kwake zilimfikia lmamu Husayn [a] alipokuwa njiani kuja Iraq mahali paitwapo Zubalah. Jambo hili liliziumiza sana fikara za Imamu [a] lakini dhamira yake isiyobadilika haikutambua njia yoyote ile nyingine; na zaidi ya hapo halikuwepo tena suala la kurudi nyuma. AIiendelea kusafiri hadi alipofika mahali paitwapo Zu-Hasm ambapo alikingiwa njia na kikosi cha jeshi la Ibn Ziyad chini ya uongozi wa mtu mmoja aliyeitwa Hurr bin Yazid Riyah. Hawa watu wa Hurr walihitaji sana maji na walikuwa wakifa kiu. Ingawa lmamu [a] alikuwa na watoto wadogo na wanawake wengi pamoja naye, aliwapa maji ya kunywa wote na akawaacha watosheke. Lakini askari hao waliyakumbuka maagizo waliyoyapewa na wakasimama kusimamisha maendeleo ya safari ya Imamu [a]. Wala hawakumruhusu arudi alikotoka. Imamu [a] alilazimishwa kupiga kambi katika wanda wa mchanga mtupu wa Karbala mnamo tarehe 2 ya mwezi wa Muharram (Mfunguo Nne) wa mwaka wa 61 Hijiriya. Siku iliyofuatia majeshi ya Yazid yalianza kumiminika katika uwanja wa vita. Sehemu hizo watu wake zililindwa vikali mno. Imamu [a] alikuwa na marafiki waaminifu sabini na wawiIi tu na upande wa Yazid ulikuwa na maelfu ya askari. Majaribio ya kudumisha amani yalifanyika kwa muda wa siku saba. lmamu [a] alikubali hata kuhama Uarabuni ili kuzuia kutokea kwa vita yoyote ile ambayo ingeliweza kutokea. Lakini katika alasiri ya tarehe 9 ya mwezi huo, mategemeo yote ya mapatano fulani yalikufa. Omar bin Saad ambaye alichukua Uamiri jeshi wa jeshi hilo kutoka kwa Hurr (baada ya Hurr kujiunga na jeshi la Imamu [a] alipata barua kutoka kwa Yazid kwa mkono wa mtu mmoja aliyeitwa Shimr ikimwamrisha kuanza vita mara moja kama Imamu Husayn [a] hakusalimu amri bila ya masharti yoyote yale. Ingawa njia zote za kufikia kwenye maji zilifungwa na watoto wa lmamu [a] walikuwa wakililia maji na hakukuweko tazamio lo lote Ia amani, lilikuwa jambo lisilowezekana kwa vyo vyote vile, kwa lmamu Husayn [a] kuyakubalia masharti ya watu waYazid. Hivyo, baada ya yote hayo aliwaomba wampe nafasi ya usiku mmoja ili aweze kumwomba Mwenyezi Mungu na vile vile pande zote mbiIi zipate nafasi ya kufikiria zaidi jambo hilo kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho. Wakati wa usiku Imamu [a] aliwakusanya watu wake pamoja na aliwahutubia akisema. "Kesho ni siku ya kujitoa mhanga. Watu hawa wana kiu ya damu yangu tu. Basi kwa nini muyahatarishe maisha yenu? Nakuruhusuni mniache na kwenda popote pale mpapendapo kwa kiza hiki cha usiku". Lakini watu hao waaminifu walisema kwa pamoja, "Hatuwezi kufanya japo kuwa tulazimike kufa mara sabini". Usiku ulikucha. Katika siku ya 10 ya Muharram, hawa marafiki wachache waaminifu wa Imamu [a] walifanya kama walivyosema na waliuthibitisha ustahiki wao. Walikuwepo watu wazee kama vile Mabwana Habib bin Muzahir, Muslim bin Ausajah, Suwaid bin Amr, Anas bin Harith, na Abdur-Rahman bin Abd-i-Rab ambao walikuwa na umri wa miaka sitini, sabini na hata themanini. Vile vile walikuwepo masahaba wachache wa Mtukufu Mtume [s] "mahafidhi" (watu waliokariri Qur'ani yote) kama vile mabwana Burair Hamdani, Kinanah bin Atiq Taghlibi, Nafi bin Hilal, Hanzalah bin Asad na watu wengine walio na elimu ya kutosha ya Qur'ani na Hadithi za Mtukufu Mtume [s] na wale ambao sala zao zisizokoma ambazo hata kiza cha mausika pia kinazishuhudia. Vile vile walikuwepo maaskari wasioogofya na kitu cho chote kile ambao majina yao yalikuwa yakitolewa mifano. Marafiki zake walipomalizika kufa, zamu iliwaangukia watu wa jamii yake. Wa kwanza wa wale walio wajibikiwa kufa alikuwa Bwana Ali Akber, mwana wa Imamu [a] aliyefanana sana na Mtukufu Mtume [s] kwa umbo lake, sauti yake na mwendo wake. Kifo cha mwana huyu kilikuwa pigo kali sana kwa Imamu [a], lakini alimpeleka wana wa Bwana Abdullah bin Jaafar kwenye uwanja wa vita na watu wengine wa jamii ya Bwana Aqil, ami yake Imamu [a]. Kisha alifuatia Bwana Qasim mwana wa nduguye Imamu Hasan [a]. Mwisho kabisa wana wa Hadhrat Ali [a] waliyatoa mhanga maisha yao. Sasa ikawa amebakia mshika bendera "Mwenzi wa Ukoo wa Bani Hasham", Bwana Abul Fadhl AI-Abbas. Imamu [a] hakumruhusu bwana huyu kwenda kupigana lakini mwishoni alimruhusu kwenda kuchota maji kwa ajili ya watoto wadogo waliokuwa wakilia kwa ajili ya kiu. Bwana Abbas alitoka kwenda mtoni na kiriba cha maji na huku ameshika bendera. Ingawa alikuwa na mizigo hiyo yote alipigana vizuri sana hata akafaulu kufika mtoni na akakijaza kiriba na akarudi. Mikono yake ilikatwa mmoja baada ya mwingine lakini alijaribu kila aliloliweza, kuwafikishia maji wale watoto wenye kiu. Akiwa bado hajafika kule waliko; mshale mmoja ulikitoboa kiriba na maji yakamwagika. Moyo wa Bwana Abbas ukavunjika na akaanguka chini kwa pigo la rungu lililompiga kichwani. Sasa Imamu Husayn [a] alikuwa peke yake, lakini bado orodha ya mashahidi haijakamilika. Aliingia hemani mwake na kuomba apewe mwanawe mdogo wa miezi sita, Bwana Ali Asghar, ambaye alikuwa akifa kwa kiu. Alimchukua mtoto huyo na kutoka naye nje kuwaendea maadui. Lakini badala ya mtoto huyu kupewa maji, koo la mtoto huyu lilipatiwa mishale mitatu na mtoto akafa. Sasa lmamu Husayn [a] yeye mwenyewe alikwenda kupambana nao, na ingawa alipata mishtuko mingi kwa kufiwa na watu wake alipouchomoa upanga wake aliwakumbusha watu siku za mabwana Hamza, Jaafar, na Hadhrat Ali [a] kwa jinsi alivyopigana kishujaa. Lakini kupoteza damu, majeraha mengi, na kuzongwazongwa na maadui mwishoni kulimuangusha. Hapa kila aina ya silaha ilitumika kumjeruhia na mwishoni upanga wa kafiri mmoja aliyeitwa Shimr ulikata kichwa cha mjukuu huyu wa Mtukufu Mtume [s] tangu nyuma ya shingo yake ili kumwongezea maumivu zaidi na kwa ajili ya laana ya Mwenyezi Mungu juu ya Shimr. Mahema ya lmamu [a] yalichomwa moto. Maiti yake iliyokuwa bila ya nguo ilikanyagwa kanyagwa na farasi za maadui. Baada ya kufariki Imamu Husayn [a], alibakia mwanawe aliyekuwa mgonjwa, aitwaye Ali Zainul Abidiin peke yake na ambaye alichukua Uimamu sasa. Imamu Ali Zainul Abidiin alitekwa pamoja na wanawake wote na watoto. Hawa Waislamu wa kujifanya tu waliziacha maiti za mashahidi hao hivi hivi bila ya kuzizika. Watu wa kabila Asad ndio waliozizika mnamo tarehe 12 Muharram mwaka huo wa 61 Hijiriyah. Kaburi tukufu la lmamu Husayn [a] huko Karbala (Iraq) bado mpaka leo lingali Kuba la Haki lizipelekeazo mionzi ya Nuru ya Mwenyezi Mungu roho zote zimchanzo Mungu. Njia mbali mbali ya kuzidhihirisia fikara zetu, 'Taziah', sadaka na vitu vingine bado vinatukumbusha mhanga wa Imamu Husayn [a] usio na kifani. Kama ulimwengu ukiyaangalia kwa makini yale aliyoyatenda Imamu Husayn [a] tuna uhakika kuwa udugu wa kweli na kujitoa kwetu kwa ajili ya kudumisha ukweli, vitakuwa tena katika iIe sura ya miaka mingi iliyopita. Watabarikiwa wale wanaomkumbuka huyo Shahidi wa Ubinadamu na kujaribu kuzifuata nyayo zake - Ameen.
|