Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(10). KESI YA MKATE

Al-Hassan b. Mahbub ameripoti: Abd al-Rahman b. al-Hajjaaj aliniambia: Nimemsikia Ibn Abi Layla akisema:

Amir ul-Muminiin a.s. ameamua kesi ambayo haikuweza kuamuliwa na mtu mwingine kabla yake.

Watu wawili waliondoka kwenda safari, wakakaa kula chakula kwa pamoja. Mmoja wao alitoa vipande vitano vya mkate na mwenzake vitatu. Alitokezea mtu mmoja akapita aliwasalimia. Nao walimkaribisha ale nao. Naye alipomaliza kula nao, aliwapa Dirham nane akisema: "Hii ni malipo ya chakula nilichokula."

Hao watu wawili walianza kuzozana juu ya Dirham hizo nane. Yule aliyekuwa na vipande vitatu alidai kuwa "Tugawane sote sawa sawa yaani Dirham nne wewe na Dirham nne mimi."

Mwenzake alisema: "Mimi lazima nipate tano na wewe tatu."

Kwa kuwa hawakuweza kuafikiana hivyo, walifikia kwa Imam Ali a.s. kuweza kupatiwa ufumbuzi. Hivyo, walimwelezea mambo yote. Imam a.s. aliwajibu."

Hili ni jambo dogo, halihitaji mzozo wala ngumi kwani suluhisho ndilo jambo bora.

"Mimi nitaridhishwa tu pale utakapotoa uamuzi wako Ewe Amir ul-Muminiin! alisema mwenye vipande vitatu vya mkate.

"Kwa kuwa wewe utaridhishwa na hukumu yangu" alisema Imam Ali a.s. "wewe utapata Dirham moja tu ambapo rafiki yako atapata Dirham saba. " alimalizia Imam a.s.

"Mungu asifiwe, " alinena, "Je itawezekanaje swala hili kuwa hivi?"

"Nilikuambia siyo?" alisema "Si ulikuwa na vipande vitatu tu vya mkate?"

"Naam! alijibu

"Yaani ni ishirini na nne (inapozidishwa) kwa tatu, alisema Imam a.s. "Kwa hiyo wewe ulikula nane, mwenzako nane,na mgeni wenu nane (kwani alitoa saba ya nane ya chakula cha mgeni wenu) na moja kwako wewe (kwani wewe ulitoa moja ya nane ya chakula cha mgeni)." Wote wawili waliondoka kwa furaha.