Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(11). SHIMO LA SIMBA

Imam Ali a.s. alipokuwa Yemen aliweza kutatua kesi nyingi mno, na mojawapo ilikuwa kama ifuatavyo:

Kulichimbwa shimo la kumnasa simba. Ikaja Simba ikatumbukia humo, na watu walizunguka lile shimo kumtazama yule simba. Mtu mmoja alikuwa amesimama ukingoni mwake, na mara ghafla akateleza, alipokuwa anaanguka shimoni, alimshika mtu aliyekuwa karibu nae. Mtu huyo alimshika mtu wa tatu, nae pia alishika wa nne. Lakini kwa bahati mbaya, wote wanne walianguka shimoni na waliuawa na simba.

Sasa je ni nani mwenye hatia? Na nani alipe fidia kati ya hao wanne?

Imam Ali a.s. alitoa uamuzi kuwa mtu wa kwanza (na familia yake) wanawajibika kulipa fidia ya theluthi ya thamani ya damu ya mtu wa pili, na hivyo, mtu wa poli na (familia yake) alipe hiyo kwa mtu wa pili, na hivyo, mtu wa pili na (familia yake) alipe hiyo kwa ajili ya mtu wa tatu na mtu wa tatu alipe hiyo kwa mtu wa nne.