Vile vile Imam Ali a.s. aliletewa kesi wakati akiwa Yemen. Msichana mmoja alimbeba msichana mwingine mabegani mwake wakati wakiwa wanacheza. Akatokezea msichana mwingine ambaye alimfinya yule msichana aliyekuwa amebebwa alianguka na shingo likavunjika, na akafa. Hivyo, Imam Ali a.s. alitoa uamuzi kuwa msichana aliyefinya ndiye anayehusika na ulipaji wa theluthi ya thamani ya damu, na msichana aliyegutuka na kuruka anawajibika theluthi yake na sehemu ya tatu haina mtu kwani ajali hiyo ilitokea wakati wao wakiwa katika michezo.
|