Kesi ifuatayo ililetwa mbele ya Imam Ali a.s. wakati akiwa bado hapo Yemen. Watu waliangukiwa na ukuta na wote walikufa. Miongoni mwao alikuwa kijakazi na mwanamke huru. Yule mwanamke huru alikuwa na mtoto mchanga aliyezaliwa kwa bwana aliye huru, na yule kijakazi alikuwa na mtoto mchanga aliyezaliwa na mtumwa. Sasa ikatokea kuwa mtoto huru hakuweza kutambuliwa na mtoto wa kijakazi. Alipiga kura baina yao; yeye alihukumu uhuru kwa yule aliyepata kura za uhuru na mtumwa kwa yule aliyepata kura za utumwa. Hapo alimfanya huru yule mtumwa na kumfanya bwana wa yule aliyekuwa huru. Vile vile alitoa uamuzi juu ya urithi wao kwa mujibu wa bwana na mtumwa wake. Hukumu zote hizo alizozitoa Imam Ali a.s. akiwa Yemen, zilisifiwa mno na Mtume s.a.w.w. Kwani zilitolewa katika uhai wake.
|