Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(14). NG'OMBE KUMWUA PUNDA

Watu wawili walifika mbele ya Mtume s.a.w.w. wakiwa wanazozana juu ya ng'ombe kumwua punda.

"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!" alisema mmoja wao, "Ng'ombe wake huyu amemwua punda wangu."

Mwendee Abu Bakr, Mwulize kuhusu hayo."

Alisema Mtume Mtukufu s.a.w.w.

Wao walimwijia Abu Bakr na kumwelezea yote.

"Je kwa nini hamkumwendea Mtume s.a.w.w. kabla ya kuja kwangu?" Aliuliza Abu Bakr.

"Sisi tumeelekezwa na Mtume s.a.w.w. mwenyewe." Wao walimjibu.

"Iwapo mnyama amemwua mnyama mwingine, basi hakuna shitaka dhidi ya mwenye mnyama (kwa ajili ya mnyama aliyeuawa)" alijibu.

Baada ya hapo, walirejea kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. na walimwelezea hivyo. Aliwajibu: "Mwendeeni Umar al-Khattab na kumwelezea kisa hicho, mwulizeni hukumu yake kuhusiana na swala hili."

Hao walimwendea na kumwelezea kisa chote. Yeye aliwauliza, "Je kwa nini mumemwacha Mtume s.a.w.w. na kunijia mimi?"

"Yeye ndiye aliyetuambia hivyo." Walimwambia.

"Je kwa nini hakuwaambia kumwendea Abu Bakr? aliuliza.

"Sisi tuliambiwa hivyo, "wao walisema, "nasi tulikwenda kwake."

"Je, aliwaambia nini kuhusu kesi hii?" aliuliza.

"Alisema kuwa mnyama anapomwua mnyama basi hapana shitaka dhidi ya mnyama mwingine. "walijibu.

"Omar alijibu: "Kwa hakika, majibu yangu pia yanakubaliana na Abu Bakr."

Wao walirejea kwa Mtume s.a.w.w. na kumpatia ripoti hiyo. Hapo Mtume s.a.w.w. "Nendeni kwa Ali ibn Abi Talib ili awatoleeni hukumu yenu."

Basi wao walimwendea Imam Ali a.s. na kumwelezea kisa chote. Imam Ali a.s. aliwauliza maswali mengi kuhusu kisa hicho.

Swali la kwanza: "Je wanyama hao wawili walikuwa pamoja wakati wa tukio hilo?"

"La, hawakuwa pamoja. "walijibu.

"Je wote wawili walikuwa wamefungwa kwa kamba?"

"La, hawakufungwa kamba," walijibu.

"Je punda alikuwa amefungwa na ng'ombe wazi?"

"Naam!" wao walijibu.

"Hivyo, Imam Ali a.s. alisema: Mwenye ng'ombe inambidi amfidie mwenye punda aliyeuawa."

Yaani kwa kifupi, Imam Ali a.s. aliwaambia: "Iwapo ng'ombe aliingia katika zizi la punda, hivyo mwenye ng'ombe lazima alipe thamani ya punda kwa mwenye punda lakini, iwapo punda aliingia katika zizi la ng'ombe, na ng'ombe akamwua punda huyo, basi mwenye punda hana haki ya kudai fidia kutoka kwa mwenye ng'ombe."

Wakati walipomwendea Mtume s.a.w.w. kumjulisha juu ya swala hilo la hapo juu na vile Imam Ali a.s. alivyoliamua, Mtume s.a.w.w. alisema: " Ali ibn Abi Talib amewaamua kama vile uamuzi wa Allah ulivyo."