Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(15). UGOMVI WA WALEVI WANNE

Katika zama za Imam Ali a.s. wanaume wanne walilewa pombe. Pombe ilipowakolea, walianza kupigana kwa visu. Kila mmoja wao alijeruhiwa vibaya sana. Mashtaka yao yalifikishwa mbele ya Imam Ali a.s. ambaye aliwaaamrisha wafungwe hadi watakapopata fahamu zao timamu. Wawili kati ya hao wanne walikufa bado wakiwa mahabusu. Familia zao (waliokufa) walimwijia Imam Ali a.s. na kudai: "Turuhusu sisi kulipiza kisasi dhidi ya watu hawa wawili, ewe Amir al-Muminiin! Kwani hao ndio waliowaua watu wetu."

"Je mmejuaje hivyo?" Imam Ali a.s. aliwauliza "labda inawezekana hawa wawili waliuawa."

"Sisi hatujui hayo," wao walijibu, "Kwa hivyo waamue kama vile Mwenyezi Mungu alivyokufundisha.

Yeye alisema: "Ubishi wa damu ya watu wawili ambao waliuawa ni wajibu wa makabila ya watu wanne baada ya kusawazishwa kwa mahesabu ya malipo ya watu wawili walio hai kwa ubishi wa damu kwa ajili ya jeraha zao."