Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(16). KUZAMA MTONI

Watu sita walikwenda kuogelea mtoni Furati. Mmoja wao alizama - akafa maji.

Watu watatu walidai kuwa wenzao wawili walimzamisha yule mtu.

Na vile vile wale watu wawili walidai kuwa wale watu watatu walimzamisha yule mtu.

Imam Ali a.s. aligawa fidia ya damu kwa sehemu tano yao. Wawili walitakiwa walipe sehemu tatu za tano kwa mujibu wa madai yao na wale watatu walitakiwa walipe sehemu mbili za tano kwa mujibu wa mashitaka dhidi yao.