Mjamzito mmoja alizini, na kesi yake ililtwa mbele ya Umar, naye aliamuru kupigwa mawe. Imam Ali a.s. alimwambia: "Lazima uwe mwangalifu mno kwa kuwa na haki ya kumwadhibu huyo, kwani itamaanisha kumwadhibu hata yule aliye tumboni mwake. Ambapo Allah s.w.t. anasema katika Quran: "Wala mbebaji hatabeba mizigo ya mwingine' (6:164)." Kwa kusikia hayo Umar alisema: "Kwa hakika katika maisha yangu sijawahi kuona swala lolote lile ambalo Abul Hasan a.s. ameshindwa kulijibu kwa ufasaha." Hapo ndipo alipouliza: "Je sasa nimfanyeje?" "Mwangalie hadi atakapojifungua, "alijibu Imam ali a.s. "Wakati atakapojifungua na wewe kumpata mtu wa kumtunza mtoto wake, hapo ndipo utakapoweza kumwadhibu." Kwa hayo, Umar alisaidiwa na Imam Ali a.s. na alishukuru kwa hayo.
|