Mzee mmoja aliona mwanamke, ambaye alishika mimba huku mzee yule aliikataa kuwa si yake, kwani alisema: "Mimi sijawahi mumwingilia huyu mwanamke tangu nimwoe," sasa mimba hiyo inatokea wapi?" Kwa kusikia hayo, Uthman bin Affan alishangaa kwa hoja hiyo, "Je mzee huyu ameumaliza ubikira wako ulipokuwa bikira?" Aliuliza Uthman. "La!" alijibu yule mwanamke. "Mtoleeni hukumu kwa mujibu wa Sharia," alitoa amri Uthman. "Mwanamke huwa na matundu mawili," alinena Imam Ali bin Abi Talib a.s." tundu la kupitia damu za mwezini na tundu la mkojo. Inawezekana kwa huyu mzee alikuwa karibu na tundu la damu ambapo alitokwa na shahawa ambazo zimemfanya huyu ashike mimba hiyo." Yule mzee alipoulizwa kuhusu hayo, alijibu: "Naam, mimi nimekuwa na mazoea ya kumwaga shahawa zangu wakati tulipokuwa tukifanya mapenzi naye lakini sijawahi kuvunja ubikira wake." "Basi mimba hiyo imetokana nayo!" alibainisha Imam Ali a.s., "na mtoto huyo ni wake tu. Mimi nadhani kuwa huyu mzee aadhibiwe kwa tuhuma zake." Uthman bin Affan alistaajabishwa mno kwa hukumu iliyofikiwa na akaitekeleza hivyo hivyo.
|