Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(2). MTUMWA ADAI BWANA WA BWANA

Imeelezwa na Kulaini na Sheikh kwa mamlaka ya Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. kuwa katika kipindi cha Ukhalifa wa Imam Ali a.s. watu wawili, mtumwa na bwana, walikuwa wakielekea kufa baada ya Hijja.

Mtumwa alifanya kosa na bwana wake alimpiga kwa kosa hilo. Hapo kwa maajabu, yule mtumwa alimwambia bwana wake. "Loh! Wewe u mtumwa wangu na wanipigia bure tu!" Ama kwa kusikia hayo, watu waliokuwa katika msafara huo walistaajabishwa na hawakuweza kuamua baina yao, na huyo mtumwa alirudia kila mara, hadi wakaingia mjini kufa.

Bwana alimwambia mtumwa: "Twende kwa Amir ul Muminiin ili tuamuliwe, "Kwa hayo Mtumwa alikubali na hivyo walitokea mbele ya Imam Ali a.s., na wakati walipokuwa wakitoa maelezo na hoja zao, wote walidai kuwa bwana. Yule mtu aliyekuwa bwana wa kweli alielezea akililia: "Baba yangu alinipeleka Hijja na wakati tulipokuwa tukirudi mtumwa huyu alifanya makosa ambayo nilimpiga. Hivyo hizi ndizo, mbinu zake za kutaka kunidhulumu mali yangu yote."

Na mtumwa pia alielezea vivyo hivyo huku akila kila aina ya viapo. Baada ya kuwasikiliza wote wawili, aliwaambia: "Nendeni na mrudi kwangu hapo kesho."

Imam Ali a.s. aliamrisha kutobolewa matundu mawili katika ukuta kiasi cha kupitisha kichwa cha mtu mmoja hadi mabega. Siku ya pili, wote wawili walifika mbele ya Imam Ali a.s., na waliamrishwa kuweka vichwa vyao katika yale matundu, kila mmoja. Baada ya hapo, Imam Ali a.s. alimwamwa ni wake, hadi kuchukuliwa kwa Umar ambaye pia aliona ugumu kufikia hukumu. Hivyo nae pia aliielekeza kesi hiyo kwa Imam Ali a.s.s. ili ipatiwe ufumbuzi ipasavyo.

Imam Ali a.s. aliwaita wanawake wote wawili na kujaribu kuwatishia. Lakini wote wawili hawakuogopa wala kushtushwa kwa hayo na walibakia katika mabishano yao- ukaidi wao!.

Imam Ali a.s. alitamka "Nileteeni msumeno mkali!"

"Je wataka kuufanyia nini?" Wote wawili waliuliza.

"Nitamkata mtoto katika sehemu mbili zilizo sawa, na nitawapatieni kipande kimoja kimoja kila mtu."

Mmoja wao alibakia kimya wakati mwingine alisema: "E Mungu wangu! Abul Hasan, iwapo hapana ufumbuzi mwingine, basi mwachie huyo mwenzangu amchukue huyo mtoto, ninamwachia." huku machozi yakimtiririka.

Imam Ali a.s. alisema: "Allah akbar! Huyu ndiye mtoto wako na wala si wa mwenzako. Iwapo angalikuwa mtoto wake, basi naye pia angalihangaika na kutapatapa."

Kwa hayo huyo mwanamke mwenye madai ya uongo alikiri kuwa yu mwongo.

Hivyo Bwana Umar alisaidiwa na alimshukuru Amir al Muminiin a.s. kwa kumwokoa katika maamuzi yake.