Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(20). FUMBO LA URITHI

Mtu mmoja alikuwa na suria (kijakazi) na alimpatia mtoto. Baadaye alitengana naye na kumwoza kwa mtumwa wake. Mmiliki wake, yule mtu, alikufa. Huyo mwanamke alikuwa huru kwa sababu ya kuwa na mtoto wa yule mtu, na vile vile yule mtoto alimrithi baba yake. Yule mtoto pia alifariki, hivyo alimrithi bwana wake kutokea mtoto wake.

Wakati hayo yanatokea, kulizuka mzozo baina yake na mwanamke (yule mtumwa). Hivyo wao walimwijia Uthman bin Affan, yeye alidai: "Huyu mwanamme ni mtumwa wangu." Na yule mwanamme alikuwa akidai: "Huyu mwanamke ni mke wangu nami sitamwachia (kutoka katika ndoa yangu)."

"Ama kwa kweli, hili ndilo swala gumu mno. "Alisema Uthman.

Katika kikao hicho, alikuwapo pia Imam Ali a.s. Yeye alisema: "Hebu mwulize huyo mwanamke kama alikuwa ameingiliana kimwili na huyo bwana baada ya kupata urithi."

"La!, hatukufuata hivyo." alijibu yule mwanamke.

"Lau ningalikuwa nimefahamu kuwa huyo bwana amefanya hivyo, basi ningelimwadhibu. "Alisema Imam a.s. " Nenda. huyo ni mtumwa wako bila ya kuwa na haki zozote juu yako. Iwapo utapenda kumweka, au kumpatia uhuru, au kumwuza, yote hayo ni haki yako."