Mwanamke mmoja alizaa kitandani mwa bwana wake, mtoto mwenye vichwa viwili na miili ikiwa imeungana kiuno kimoja tu. Kwa hayo, wanafamilia wote walistaajabishwa na hawakuelewa iwapo ni watoto wawili au ni mmoja. Hivyo wao walimwendea Imam Ali a.s. kuhusu kujua iwapo ni mmoja au wawili na hukumu za sharia kuhusiana na swala hilo. Imam Ali a.s. alimwambia. "Mtazameni pale aendapo kulala. Jaribuni kuuamsha mwili mmoja na kichwa chake. Iwapo miili na vichwa vyote viwili vitaamka kwa pamoja, basi wao ni binadamu mmoja tu. Na iwapo mmoja ataamka na mwingine atabakia amelala, basi mutambue kuwa wao ni binaadamu wawili tofauti na watakuwa na haki za watu wawili katika urithi."
|