Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(23). UWEUPE WA YAI

Mwanamke mmoja alimwashiki kijana mmoja na alifanya kila jitihada ya kumvutia kwake, lakini yule kijana alimkatalia kabisa kabisa. Basi kwa hasira zote aliondoka na akachukua yai la kuku. Huyo mwanamke alijipaka uweupe wa yai juu ya nguo zake, huku akifanya madai ya kunajisiwa na yule kijana wa kiume, hadi akaletwa mbele ya Imam Ali a.s.

Huyo mwanamke alidai: "Huyu ndiye kijana aliyeninajisi."

"Hii hapa shahawa (manii) yake juu ya nguo zangu." Aliendelea kusema yule mwanamke.

Kwa hayo, yule kijana alilia huku akila viapo vya kutotenda uovu huo.

"Nileteeni maji yaliyo na moto kabisa," Imam Ali a.s. alimwambia Qambar.

Maji moto kabisa yalipoletwa mbele yake, aliamrisha ya mwagiwe juu ya nguo za yule mwanamke. Yalipomwagiwa juu ya nguo za yule mwanamke, kulianza kubadilika rangi kuwa nyeupe ya mayai.

Ili kuthibitisha hayo, watu wawili walionja iwapo ni kweli, nao walisadikisha kuwa yalikuwa ni uweupe wa mayai.

Papo hapo Imam Ali a.s. aliamrisha yule kijana aachiliwe huru na yule mwanamke alipewa adhabu ya kuchapwa sana kwa kosa la kusingizia.