Ushahidi kamili ulitolewa mbele ya Umar dhidi ya mwanamke mmoja aliyekuwa ameona akizini pamoja na mtu mwingine mbali na mume wake hapo jangwani. Umar papo hapo alitoa amri ya kuuawa kwake kwa kupigwa mawe kwani alikuwa na mume wake halali. Kwa hayo alisema yule mwanamke: "Ewe Milipoishiwa na maji niliomba anisaidie maziwa, lakini yeye alitaka nijitolee kwake badala ya maji. Nilimkatalia kata kata. Ulifika wakati ambapo maisha yangu yalikuwa yanataka kukatika, ndipo hapo nilipojisalimisha mbele yake bila ya ridhaa yangu." "Allahu akbar!" alisema Imam Ali a.s. kwani aliye lazimishwa au kuzidiwa hana kosa wala hana dhambi kea mujibu wa Aya ya 123 katika Sura al-Baqarah." Umar aliyasikia hayo kwa makini na alimwachilia huru yule mwanamke.
|