Imeripotiwa na kulaini na Sheikh kwa mamlaka ya Zazaan kuwa wanaume wawili waliweka amana yao kwa mwanamke mmoja kwa masharti kuwa asiwarudishie amana hiyo hadi wao wote wawili waje kwa pamoja. Baada ya muda kupita, mmoja wao alimwendea yule mwanamke na kumwambia: "Nipe ile amana yetu tuliyokuachia kwani mwenzangu amefariki. "Yule mwanamke alimpa amana hiyo kwa kuyaamini ayasemayo. Baada ya muda kupita, akaja yule mtu wa pili akielezea vile alivyokuwa ameelezea mtu wa kwanza. Mtu huyo alipoelezwa yaliyotokea, alimshtaki mwanamke kwa Bwana Umar, ambaye alishindwa kutoa hukumu, hiyo alielekeza mbele ya Imam Ali a.s. kwa kupatiwa hukumu. Imam Ali a.s. aliwaita wote na akamwambia yule mwanamme: "Hiyo amana ipo kwangu, na mimi sitaweza kuitoa kwa yeyote yule hadi muje wote wawili kwa pamoja,kwa mujibu wa masharti yenu wenyewe!" Kwa hivyo,aliendelea Imam a.s.: "Nenda ukamlete mwenzako ili niwarudishie amana yenu." Mtu huyo aliaibika na akaondoka zake.(Inaonekana kuwa hao walikula njama ya kutaka kumtapeli mwanamke huyo).
|