Asbagh bin Nabata ameripori kuwa watu watano waliotuhumiwa kwa kuzini, waliletwa mbele yake Umar, ambaye alitoa amri ya papo hapo ya kupigwa mawe hadi kufa kwao. Imam Ali a.s. alipoyasikia hayo, alisema kuwa hukumu hiyo haikuwasahihi. Hapo ndipo alipokutanana kuwahoji kila mmoja wao pekee na akatoa hukumu kama ifuatavyo: Mtu wa kwanza akatwe kichwa, wa pili apigwe mawe hadi kufa kwake, watatu achapwe viboko na nusu ya adhabu kamili kwa mtu wa nne. Ama mtu wa tano aliachiliwa huru baada ya kuadhibiwa kikawaida tu. Umar alimwomba Imam Ali a.s. amwelezee juu ya uamuzi huo wa kiajabu. "Mtu wa kwanza ni Zimmi[3] ambaye amezini pamoja na mwanamke Muislamu; mtu wa pili ni yule aliyeoa ambaye kwa mujibu wa sharia za Di ni kurajimiwa[4] ; mtu wa tatu ni yule asiyeoa achapwe viboko; mtu wa nne ni mtumwa ambaye ataadhibiwa nusu ya adhabu kamili kwa mujibu wa sharia za Sin, na wa tano ni nusu-mwendawazimu hivyo anastahili adhabu ya kawaida kwa kosa kama la wenzake." Umar alisema: "Nisije kuishi katika nchi ambapo Abul Hasan hayupo kuyatatua matatizo kama hayo." [3] Zimmi ni mtu alupaye kiasi fulani cha fedha kwa Dola ya Kiislamu kwa ajili ya kupatiwa usalama wa maisha yake. [4] Rajm yaani kupigwa mawe hadi kufa.
|