Mtu mmoja alimtuhumu mke wake kwa zinaa, walifika kwa Uthman bin Affan kwa kumwita mke wake 'mzinifu.' Mwanamke yule alijibu: "Wewe ni mzinifu zaidi yangu mimi!" Kwa kusikia hayo, Umar aliamrisha wote wawili wachapwe viboko. Imam Ali a.s. alipoyasikia hayo, alimwambia Umar asiwe akifanya haraka katika kufikia uamuzi wake kwani si sahihi hivyo. Imam Ali a.s. alisema: "Kwa maneno ya mwanamke mwenyewe, amekiri kwa yeye ni mzinifu ambapo amestahili adhabu mara dufu. Adhabu moja ni kule kukiri kwake kwa zinaa na pili ni kule kumsingizia mume wake. Lakini adhabu yake ya uzinifu itakuwa nusu kwa sababu hajakiri mara nne ambavyo inavyotakiwa katika sharia za Din. "Ama mume wake" aliendelea Imam a.s. kusema: "Ataachiliwa huru kwani yeye hajakiri wala hakuna ushahidi dhidi yake." Uthman alikiri hayo, na kuhukumu vile Imam ali a.s. alivyoelezea.
|