Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(37). MBINU MPYA ZA ZINAA

Mwanamke mmoja alimpenda na kumwashiki mwanamme mmoja, hivyo alitafuta mbinu za kuweza kutimiza hamu yake pamoja nae. Alilala kitandani mwa yule mwanamme akijigeuza kama kijakazi wake.

Wakati yule meanamme alifika kitandani, akamuona mwanamke amelala, na hivyo hakutaka kupoteza fursa hiyo, akazini nae.

Kesi hiyo ilipofikishwa mbele ya Imam Ali a.s., alimwamrisha kuwa mwanamke yule aadhibiwe hadharani wakati mwanaume arajimiwe katika faragha kwa sababu kosa lake lilikuwa dogo kuliko la mwanamke yule, kwani yeye ndiye chanzo cha kosa hilo. Na huyo mwanamme ameadhibiwa kwa sababu alikwisha fahamu na kutambua yule mwanamke ama sivyo, angaliachiwa huru bila ya kuadhibiwa.