Mtu mmoja aliyekuwa na majeraha mwilini alishitakiwa mbele ya Imam Ali a.s. ambaye alitoa hukumu ya kusubiri hadi atakapopona kabisa. Baada ya kipindi, alipopona, aliadhibiwa kikamilifu. Kesi moja ililetwa mbele ya Mtume s.a.w.w. ya mgonjwa istiska (tumbo la maji) kazini kwa nguvu pamoja na mwanamke yule, ambapo yeye alikuwa hajaoa. Hapo Mtume s.a.w.w. aliagiza makuti mia moja na akachapwa kwa mara moja.[5] [5] Hakimu kabla ya kutoa hukumu inambidi atambue hali na wakati wa tukio hilo.Iwapo mgonjwa anayo matumaini ya kupona,basi asubiriwe hadi atakapo pona ndipo adhabu itolewe na iwapo hatapona,basi inaweza kutekelezwa kama vile Mtume s.a.w.w. alivyofanya.
|