Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(41). ZINAA USINGIZINI

Mtu mmoja alimleta mtu mwingine mbele ya Abu Bakr akidai kuwa: "Huyu mtu amesema kuwa ametokwa na manii kwa kuota kuwa amezini pamoja na mama yangu."

Khalifa alishangaa kwani hakuwa na lakujibu.

Imam Ali a.s. wakati huo alikuwa msikitini, alisema "Mtu aliyeilezea ndoto yake, asimame juani na adhabu zake zipatwe kivuli chake kwani alizini akiota tu, na vile vile achapwe kiboko kimoja au viwili ili akome kuwasumbua watu kwa maneno ya kipuuzi."