Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(5). MTOTO MWENYE RANGI TOFAUTI

Mnigro mmoja alimwijia Bwana Umar. Mke wake alikuwa mweusi. Yeye alimwambia Umar kuwa yeye pamoja na mke wake ni mweusi, lakini amezaa mtoto mwenye rangi ya kunde kinyume na rangi yao. Yeye pia alisema kuwa haina shaka kuwa mke wake amezini na mtu mwingine ambaye ana rangi ya mtoto huyo.

Bwana Umar hakuwa na majibu ya swala hilo hivyo alielekeza kesi hiyo kwa Imam Ali a.s. ili kupatiwa ufumbuzi wake.

Imam Ali a.s. alimwuliza Mnigro huyo: "Je iwapo nitakuuliza swali, utanijibu kwa usahihi?

Mnigro huyo alimjibu: "Ndiyo Bwana! Kwa uwezo wangu wote na kwa usahihi."

Imam Ali a.s alimwuliza huyo Mnigro: "Je ulimwendea mke wako yaani ulimwingilia yeye akiwa katika vipindi vyake vya mwezini?"

Mnigro alijibu: "Ndiyo Bwana, nafikiri nilifanya hivyo."

Kwa majibu hayo, Imam Ali a.s. alimwambia: "Rangi ya mtoto ni matokeo ya tendo lako hilo. Kwa hivyo, wewe ndiwe mwenye hatia na wala si mke wako." Mnigro aliaibika na akajiondokea.