Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(6). MTU MLEVI

Kesi hii ya kwanza kutolewa hukumu baada ya kifo cha Mtume s.a.w.w. na ni ya aina yake.

Bwana Kulaini ameripoti kwa mamlaka ya Imam Ja'afar as-Sadiq a.s. kuwa: "Katika zama za Abubakar mlevi mmoja aliletwa ili ahukumiwe kisharia.

Hata hivyo, mtu alisema: "Mimi ingawaje ni Mwislamu, lakini naishi miongoni mwa watu ambao hawajui kuwa pombe ni haramu katika Islam na wala mimi sikuwahi kusikia hivyo."

Kwa hayo, Abubakar alishangazwa na hali hiyo na akaona vigumu kutoa hukumu. Wengine waliokuwa pamoja nae walimwambia, mwulizie Imam Ali a.s. kwani ni yeye pekee atakayeweza kujibu swala hili.

Imam Ali a.s. aliwatuma Waislamu wawili waaminifu katika makazi ya Muhajirin na Ansar na kuwaambia "Wawaulize iwapo yeyote miongoni mwao amemsomea (huyu mtu) Aya ya Quran zinazoharamisha pombe au iwapo alishawahi kuwambia Hadith za Mtume s.a.w.w. Iwapo yeyote miongoni mwao atatoa ushahidi basi atatolewa huku na iwapo hatapatikana mtu basi ataambiwa aombe msamaha na kutubu, hivyo ataachiwa huru."

Hao watu wawili walirejea kwa majibu ya kutoambiwa kwa mtu huyo chochote kile kihusianacho na kuharamishwa kwa pombe.

Kwa matokeo hayo, Imam Ali a.s. alimkanya vikali mtu kulewa kwake tena na alitubu huyo mtu. Aliachwa huru.