Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(7). MTOTO AITWA 'DINI IMEKUFA'

Imeripotiwa kuwa Siku moja Imam Ali a.s. aliingia msikitini kufa, akamwona kijana mmoja akilia mno huku akiwa amezungukwa na watu waliokuwa wakimhurumia. Imam Ali a.s. aliwauliza hoja ya kilio hicho.

Kijana huyo alisema: "ya Amir Ul-Muminiin, Shurayh, Qadhi wetu amenihukumu kesi dhidi yangu na kuninyima haki yangu."

Imam Ali a.s. alimwuliza: "Je kesi yako inahusiana na jambo gani?"

"Watu hawa" alisema kwa kuwaelekeza watu waliokuwapo, "walimchukua baba yangu katika safari pamoja nao. Wao wamerejea lakini yeye hakurejea. Mimi niliwauliza kuhusu baba yangu, nao walinijibu kuwa amefariki safarini. Nami niliwauliza kuhusu mali aliyokuwanayo, nao waliniambia: 'Sisi hatujui lolote lile kuhusu mali yake hiyo! Hapo ndipo Qadhi Shurayh alipowaambia wale viapo kwa maelezo yao, nao walikula viapo, hapo ndipo aliponiambia kuwa nisiwabughudhi hao watu au kuwaingilia katika mambo yao.

Imam Ali a.s. alimwambia Qambar: "Waite na wakusanye watu na shurtat al-Khamis [1]

Aliketi na kuwaita wale watu (waje mbele yake) pamoja na yule kijana. Alimwambia yule kijana aelezee, naye alielezea vile vile kama awali huku akilia, kwa kusema: "Kwa kiapo cha Mwenyezi mungu, mimi ninawashtaki hawa watu kwa kumwua baba yangu. Ewe Amiral-Muminiin. Wao walimdanganya na kumchukua pamoja nao ili wao waweze kunyang'anya mali yake."

Imam Ali aliwageukia hao watu kwa kuwauliza nao walimjibu vile vile kama vile walivyokuwa wamemjibu Qadhi Shurayh: "Huyo bwana alikufa tu na wala hatujui kuhusu mali yake."

Baada ya hapo, aliwatazama usoni mwao na kuwaambia: "Je mnafikiriaje? Je mnadhani kuwa mimi sijui lolote lile mulilomfanyia huyo baba wa kijana huyu? Basi itamaanisha kuwa mimi nitakuwa na ilimu kidogo kabisa."

Alitoa amri ya kutenganishwa, nao walitenanishwa humo msikitini. Kila mmoja alisimamishwa kwenye kizingiti. Alimwamrisha Ubayd Allah b. Abi Rafi, mwandishi wake wakati huo, aketi karibu hapo. Na hapo alimwita mmoja wao, na alimwambia: "Niambie ni siku gani mulipotoka nyumbani kwa ajili ya safari pamoja na babake huyu kijana? Na uyaseme hayo bila ya kuipaza sauti yako."

"Siku fulani na fulani "yeye alijibu.

"Yaandike hayo," alimwambia Ubayd Allah.

"Ulikuwa mwezi gani" aliuliza Imam Ali a.s.

"Ulikuwa mwezi fulani fulani " alijibiwa.

"Yaandike hayo pia," alisema.

"Ulikuwa mwaka gani?" "Ulikuwa mwaka fulani."

"Yaandike,

Ubayd Allah alikuwa akiyaandika yote hayo.

"Kwa magonjwa gani alifariki? aliuliza

"Kwa ugonjwa fulani fulani" alijibiwa.

"Mahala gani alifariki?"

"Mahala fulani fulani"

"Nani aliyemwosha na kumvisha sanda?"

"Fulani fulani,"

"Mulimvisha sanda ya nini?"

"Kwa kitu fulani fulani,"

"Nani aliyesalisha sala ya maiti?"

"Fulani fulani."

"Ni nani, aliyemteremsha kaburini?"

"Fulani fulani.

Ubayd Allah alikuwa akiyaandika yote hayo yaliyokuwa yakiulizwa na kujibiwa. Walipofikia swali la kaburi, Imam Ali a.s. alitoa Takbiri kwa nguvu kiasi kwamba kila mtu aliyekuwapo hapo Msikitini alisikia. Hapo akaamrisha yule mtu arejeshwe mahala pake.

Baada ya huyo, alimwita mtu wa pili akae karibu naye. Imam Ali a.s. alimwuliza maswali hayo hayo aliyomwuliza mtu wa kwanza, majibu yake yote kwa pamoja yalikuwa kinyume kabisa na ya yule wa kwanza. Hayo yote pia yalikuwa yakiandikwa na ubayad Allah. Alipomaliza mtu huyo kutoa majibu yake, Imam Ali a.s. alitoa Takbir kwa sauti kiasi kwamba wote walisikia. Aliamrisha wote wawili wafungwe kifungo lakini wasubiri kwenye mlango wa Msikiti.

Imam Ali a.s. alimwita mtu wa tatu na kumwuliza vile vile alivyowauliza waliotangulia. Naye pia alijibu kinyume na wenzake wawili. Imam Ali a.s. aliamrisha achukuliwe kwa wenzake wawili.

Hapo alimwita mtu wa nne. Maneno yake yalitatanisha na kubabaisha. Imam Ali a.s. alimwonya na kumtishia. Mtu huyo alikiri kwa wenzake walimwua yule bwana na kuchukua mali na kwamba alizikwa mahala fulani fulani karibu na mji wa Kufa. Imam Ali a.s. alitoa Takbir, na kuamrisha achukuliwe mahabusu.

Kwa mara nyingine tena, Imam Ali a.s. alimwita mmoja wa wale waliokwisha kuulizwa, na kumwambia: "Wewe ulidai kuwa mtu huyo alikufa akiwa kitandani. Ambapo nyie mumemwua. Niambie ukweli kabisa kuhusu hali halisi, ama sivyo nitakuadhibu vikali kiasi kwamba utakuwa ni fundisho kwa wengine kwamba niwe nikiambiwa ukweli mtupu." Mtu yule alikiri kumwua yule bwana kama vile alivyokuwa ameelezea mwenzake.

Hapo aliwaita wote waje mbele yake, nao wote walikiri kumwua yule bwana. Imam Ali a.s. aliwaamrisha baadhi ya watu wake waondoke na hao hadi pale walipokuwa wameizika mali ya bwana, hivyo kumpa mtoto wake marehemu.

Imam Ali a.s. alimwuliza yule kijana: "Je umetaka kufanyiwa nini hawa watu kwani umekwishajua kile walichomtendea baba yako."

"Mimi nataka Mungu atuamue siku ya Qiyama na hivyo ninawaachilia humu duniani." alijibu kijana.

Kwa hivyo, Imam Ali a.s. hakuwaadhibu kwa mujibu wa adhabu za kuuwa bali aliwaadhibu vikali kwa madhambi yao.

Qadhi Shuryh alistaajabishwa kwa uamuzi huo wa Imam Ali a.s. na hakuweza kujizuia kwa kumwuliza Imam Ali a.s. "Ewe Amir ul-Muuminiin! Je umewezaje kufikia uamuzi huu?"

Imam Ali a.s. alimjibu: "Mtume Daudi a.s. aliwapita baadhi ya watoto waliokuwa wakicheza na aliitwa mmoja wao, 'Dini imekufa'. Hapo alikuwa akiwajibu. Mtume Daudi a.s. aliwaendea, na kumwuliza mmoja, "Ewe, kijana, je unaitwa nani?"

'Jina langu ni Dini imekufa,' alijibu.

'Je ni nani aliyekupatia jina hilo?" aliuliza Mtume Daud a.s.

Alijibu, "Mama yangu, aliye nyumbani. 'Ndipo Mtume Daud a.s. alipomwambia, twende utupeleke nyumbani kwenu. "Hivyo walikwenda hadi nyumbani kwao na kumwita nje mama yake, 'Ewe mama je, mtoto wako anaitwa nani?' Jina lake ni Dini imekufa.' alijibu huyo mama. Mtume Daudi a.s. aliendelea kumwulizia,'Je ni nani aliyempatia, jina hilo? Huyo mama alijibu, "Baba yake mzazi."

Imam Ali a.s. alimwuliza, "Je ni kwa sababu zipi alimpatia jina hilo?" Huyo mwanamke alijibu: nilipokuwa mja mzito, baba yake alikwenda safari pamoja na baadhi ya watu. Wale watu wote walirejea salama lakini yeye hakurejea. Mimi nilijaribu sana kuwauliza kuhusu bwana wangu lakini wao walijibu kuwa alifariki safarini. Vile vile niliwaulizia kuhusu mali aliyokuwa nayo, lakini wao walisema kuwa hakuwa na chochote na hivyo wao hawakujua chochote kile! Vile vile niliwauliza iwapo alisema chochote katika usia wake. Nao walisema kuwa aliwaambia mtoto atakayezaliwa aitwe Dini imekufa, na hivyo ndivyo nilivyomwita hivyo kwani sikutaka kwenda kinyume na usia wake.'

Hapo Mtume Daudi alipomwuliza yule mwanamke, "Je unawajua watu hao?" Mwanamke alijibu 'Naam!' Wale wote waliochukuliwa nesi hiyo ilipokuja mbele ya Imam Ali a.s. alitoa hukumu ya mtu wa kwanza mwenye amana ya Dinar mbili alipwe Dinar moja na wagawane sawasawa na mtu wa pili ile Dinar ya pili.[2]

 

Notes:

[1] Kwa mujibu wa Ahmad b.Abi Abd Allah al-Barqi,shurtat al-Khamis walikuwa ni wafuasi elfu sita wa Imam Ali a.s. ambao wamekula viapo vya kumtumikia hadi kufa kwao,Al-Rijal (Teheran 1342 A.H.),wao vile vile wanasemekana kuchanganyikana na wanamgambo,polisi na wapiganaji wa mstari wa m,bele.

[2] Mtu aliyewekesha Dinar mbili anayo Dinar moja ililsalimika hata kama tutachukulia kuwa Dinar yake moja imeibiwa,ambapo mtu wa pili,iwapo itakuwa Dinar yake moja ndiyo iliyoibiwa,basi hatabakia na chochote. Kwa kuwa uwizi uliathiri Dinar ya pili,hivyo wote waligawana faida na hasara yake.