Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
(8). KUZALIWA KWA MTOTO WA MIEZI SITA

Mwanajeshi mmoja aliporejea nyumbani kwake alikuta mke wake amezaa mtoto wa kiume ambapo yeye anadai kuwa aliishi nao kwa miezi sita tu. Mwanajeshi huyo alimkatalia huyo mtoto,na kupeleka kesi yake mbele ya Umar,ambaye alitoa hukumu ya kupigwa mawe huyo mwanamke (mama mtoto).

Kwa bahati Imam Ali a.s. pia alikuwapo hapo, alisema: "Iwapo utapingana na kitabu cha Allah s.w.t. basi tutaikhatalafiana. Allah s.w.t. amesema katika Quran tukufu: "Nabeba mimba yake hata kumwachisha ziwa (uchache wake) ni miezi thelathini. -(46:5). Vile vile Allah s.w.t. amesema katika Quran Tukufu: "Wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili.......'(2:233). Wakati mwanamke alipotimiza kunyonyesha kwa miezi thelathini.... Kwa sasa (yeye ametimiza tu) wajibu (wa kumnyonyesha) kwa miezi sita (na hivyo hawezikuuawa)."

Umar alimwachilia huru yule mwanamke na alikubaliana na uamuzi huo. Ma-Sahaba walifuata hilo na vile vile al-tabi'un pia wameitumia hadi leo.