
Zama Zitakazofika
Amiraly M.H. Datoo (PO Box 838 Bukoba, Tanzania)
Hadithi hii ilisomwa na: Sheikh Akmal Hussein Taheri - Bukoba.
Amesema Mtume sa.w.w. kuwa: Utafika wakati katika Ummah wangu ambapo:
1. Nyuso za watu zitakuwa za kibinadamu lakini nyoyo zao zitakuwa za kishetani na mfano wao utakuwa kama mnyama mwenye kudhuru na ambaye daima hutaka damu tu
2. Kamwe hawazuii watu kutotenda maovu bali wao wenyewe watakuwa wakiyatenda hayo hayo
3. Iwapo watu kama hao watafuatwa basi watawatumbukiza watu katika hali ya mashaka
4. Iwapo utaongea nao, basi daima watakukadhibisha
5. Na iwapo utajaribu kujitenga nao basi wataanza kukusengenya
6. Kwao Sunnah ni bida'a na bida'a kwao ni Sunnah mifano ni mingi kama hii ya Mi'raji, uzawa wa Mtume sa.w.w. , n.k.
7. Watu walio na heshima kwao ndio wanachukuliwa kuwa waovu
8. Na wale walio waovu miongoni mwa watu ndio wanaoheshimiwa na kutukuzwa
9. Waumini miongoni mwao ni watu waliokandamizwa
10. Ambapo waovu ndio wanaotukuzwa kwao
11. Watoto wao hawana heshima wala tabia njema
12. Na wake zao watakuwa waovu kiasi kwamba waume zao watakuwa wamewachoka wake zao na watajaribu kujiepusha nao. (Wanawake kutovaa hijabu na mavazi ya heshima yenye kuwasitiri wao, kujipamba na kujirembesha kwa ajili ya wengine, kupeana mikono na wanaume wasio waume zao. Ama wanaume pia hawapo nyuma katika masuala kama haya kwani utayasikia kuwa wanaume wengine wanao wake wa pembeni hata bila ndoa, vile vile utawasikia wauza pombe kuwa biashara yao inaanguka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ati wanywaji wa pombe wengi ni Waislamu
13. Maulamaa wao hawawaongozi kwa mema na wala hawawakatazi dhidi ya maovu yaliyo miongoni mwa Waumini (ati kwa sababu za fedha na hofu ya maslahi yao kwamba yeye hujiinamisha mbele ya matajiri na kuwadhalilisha masikini
14. Kuomba msaada wao ni kujidhalilisha
15. Na kwa kuwaomba msaada wakati wa shida, basi huwadharau waombaji
16. Na kuomba chochote kutoka kwa watu kama hawa ni umasikini na ufukara
17. Na utakapofika wakati kama huo, basi Allah swt hatawanyeshea mvua hata kwa tone moja wakati utakapofika msimu wa mvua na badala yake kutakuwapo na mvua pasi na msimu wake. Sasa jee mvua zisizo za msimu zinasaidia vipi ? Jee hii si dalili ya adhabu na maafa ?
18. Na watu watasalitiwa na wadhalimu waovu kabisa
19. Ili watu hao watawapeleka watu kuelekea makali ya adhabu
20. Nyakati hizo watu wataomba dua lakini hazitakubaliwa
21. Nyuso za watu zitakuwa za kibinadamu lakini nyoyo zao zitakuwa za kishetani na mfano wao utakuwa kama mnyama mwenye kudhuru na ambaye daima hutaka damu tu
22. Kamwe hawazuii watu kutotenda maovu bali wao wenyewe watakuwa wakiyatenda hayo hayo
23. Iwapo watu kama hao watafuatwa basi watawatumbukiza watu katika hali ya mashaka
24. Iwapo utaongea nao, basi daima watakukadhibisha
25. Na iwapo utajaribu kujitenga nao basi wataanza kukusengenya
26. Kwao Sunnah ni bida'a na bida'a kwao ni Sunnah mifano ni mingi kama hii ya Mi'raji, uzawa wa Mtume sa.w.w., n.k.
27. Watu walio na heshima kwao ndio wanachukuliwa kuwa waovu
28. Na wale walio waovu miongoni mwa watu ndio wanaoheshimiwa na kutukuzwa
29. Waumini miongoni mwao ni watu waliokandamizwa
30. Ambapo waovu ndio wanaotukuzwa kwao
31. Watoto wao hawana heshima wala tabia njema
32. Na wake zao watakuwa waovu kiasi kwamba waume zao watakuwa wamewachoka wake zao na watajaribu kujiepusha nao. (Wanawake kutovaa hijabu na mavazi ya heshima yenye kuwasitiri wao, kujipamba na kujirembesha kwa ajili ya wengine, kupeana mikono na wanaume wasio waume zao. Ama wanaume pia hawapo nyuma katika masuala kama haya kwani utayasikia kuwa wanaume wengine wanao wake wa pembeni hata bila ndoa, vile vile utawasikia wauza pombe kuwa biashara yao inaanguka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ati wanywaji wa pombe wengi ni Waislamu
33. Maulamaa wao hawawaongozi kwa mema na wala hawawakatazi dhidi ya maovu yaliyo miongoni mwa Waumini (ati kwa sababu za fedha na hofu ya maslahi yao kwamba yeye hujiinamisha mbele ya matajiri na kuwadhalilisha masikini
34. Kuomba msaada wao ni kujidhalilisha
35. Na kwa kuwaomba msaada wakati wa shida, basi huwadharau waombaji
36. Na kuomba chochote kutoka kwa watu kama hawa ni umasikini na ufukara
37. Na utakapofika wakati kama huo, basi Allah swt hatawanyeshea mvua hata kwa tone moja wakati utakapofika msimu wa mvua na badala yake kutakuwapo na mvua pasi na msimu wake. Sasa jee mvua zisizo za msimu zinasaidia vipi ? Jee hii si dalili ya adhabu na maafa ?
38. Na watu watasalitiwa na wadhalimu waovu kabisa
39. Ili watu hao watawapeleka watu kuelekea makali ya adhabu
40. Nyakati hizo watu wataomba dua lakini hazitakubaliwa.