 |
MTUKUFU MTUME (S.A.W.) ASEMA
- "Ee Allah! Hawa (Ali, Fatima, Hasan na Husain) ndio AhlulBait wangu, basi watoharishe kwa tohari kamili."
- "Husain anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husain..."
- "Hao (Hasan na Husain) ni maua yangu katika dunia."
- "Ewe Mwanangu (Husain)! Mwili wako ni mwili wangu na damu yako ni damu yangu;"
- (Ewe Husain), wewe u Sayyid, mwana wa Sayyid, na ndugu wa Sayyid; wewe u uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu) mwana wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu) na ndugu wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu); na baba wa uthibitisho tisa ambao wa tisa wao ni Qaim wao ambaye atakuwa al-Mahdi.
- "Hasan na Husain ni Masayidi wa Vijana wa Peponi."
- "Ewe Mola wangu! Mpende yule ampendae Husain."
- "Adhabu atakayoipewa yule mwuaji wa Husain huko Motoni itakuwa sawa na nusu (nzima) ya adhabu yote watakayoipewa wenye dhambi waulimwengu."
- " Allah hujirafikisha na wale wajirafikishao na Husain yu adui wa wale walio maadui zake."
|