Ahlul-Bayt (A.S.) Assembly ya Tanzania (ABATA) ina furaha kutoa kitabu kama hicho cha Majlis kwa watu wazungumzao Kiswahili. Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Mwenyekiti wa ABATA, amekichagua kwa ajili ya madhumuni hiyo kitabu kiitwacho "Muqaddamah al-Majalis al-Fakhirah fi Ma'atim al-Itrah at Tahirah" kilichoandikwa na mwanachuoni mashuhuri wa dini na mtunzi, marehemu Allamah Sayyid Abdul Husain Sharafud-din al-Musawi, wa Jabal Amil (Lebanon). Shaykh Musabah Shaban Mapinda, wa Dar-es-Salaam, kwa ushauri wa Mwenyekiti wa ABATA amefanya tarjuma ya kitabu hiki kutoka Kiarabu kwenda kwenye Kiswahili, knachoitwa "Maombolezo ya Kifo cha Imam Husain (a.s.)." Hiki ni kitabu cha pili ambacho kinatolewa na Ahlul-Bayt (a.s.) Assembly ya Tanzania; na tunayo furaha kubwa kwa kutoa kitabu cha Majlis ambacho ni cha kwanza katika lugha ya Kiswahili. Allah Subhanahu wa Ta'ala atoe malipo yake kwa mtunzi, mfasir na wale wote ambao wamesaidia katika uchapishaji wake kwa njia yoyote. Wa ma Tawfeeqi illa Billah
|