Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
MAJLIS YA TANO YAH: KUMTOLEA SADAKA MAITI

Hapana shaka kwamba, ni jambo zuri kuwatolea sadaka maiti wa Waumini kwani jambo hilo alilifanya Mtume (s.a.w.) na akaamuru lifanywe.

Ndani ya sahihi mbili (Bukhari na Muslim) imepokewa toka kwa Bibi Aisha amesema: "Sikupata kumuonea wivu mwanamke ye yote miongoni mwa wakeze Mtume kuliko nilivyomuonea wivu Bibi Khadija ambaye hata sikuwahi kumuona, lakini Mtume alikuwa akimtaja sana (Khadija) na wakati mwingine alikuwa akichinja kondoo na kumkatakata vipande vipande kisha huvipeleka kwa jamaa za Khadija kuwa ni sadaka, basi wakati mwingine nilimuambia Mtume (s.a.w), "Kama kwamba katika Dunia hii hakupata kuweko mwanamke isipokuwa Khadija, basi Mtume husema hakika alikuwa ni mwanamke wa pekee bora (katika wake nilioowa) na wala hajakuwepo wa mfano wake na kwake yeye Khadija nilipata watoto".

Hadithi hii inatuonyesha kwamba ni jambo zuri kutowa sadaka kwa marafiki au jamaa wa maiti.

Taz. Sahihi Bukhari Juz. 2 Uk. 207.

Naye Imam Muslim ameandika kwamba, mtu mmoja alifika kwa Mtume (s.a.w.) akasema: "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika mama yangu amefariki na wala hakuacha usia, je, atapata malipo iwapo nitamtolea sadaka? Mtume akasema: "Ndiyo".

Taz. Sahihi Muslim Juz. 1 Uk. 372.