Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
KUZALIWA KWA AL-IMAM HUSEIN BIN ALI (A.S.)

Al-Imam Husein (a.s.) amezaliwa tarehe tano Mwezi wa Shaaban Mwaka wa nne Hijiriyah.

Baada ya kuzaliwa kwake alishuka Jibril (a.s.) akiwa na kundi la Malaika wapatao Elfu Moja, wakampongeza Mtume (s.a.w.).

Mtume (s.a.w.) alifurahi sana kwa kuzaliwa kijana huyu, na akawa amempa jina Ia Husein.

Imepokewa kutoka kwa Ummul-Fadhl mkewe Bwana Abbas Bin Abdil-Mutalib amesema; "Niliota ndoto kabla Husein hajazaliwa, nikaona kama kwamba kipande cha nyama ya mwili wa Mtume kimewekwa mapajani mwangu basi nikamsimulia jambo hilo Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mtume akasema: "Naona kuna kheri iwapo ndoto yako itakuwa ya kweli, kwani Fatma atazaa mtoto wa kiume nami nitakupa wewe umlee".

Anaendelea kusimulia Ummul-Fadhli anasema: "Basi mambo yakawa kama alivyosema Mtume (s.a.w.) na akanipa Husein nimlee".

Siku moja nikaja naye kwa Mtume (s.a.w.), wakati Mtume (s.a.w.) akiwa anambusu Husein, alikojoa na likaruka tone la mkojo kwenye nguo ya Mtume (s.a.w) nikamshika Husein (a.s.) ili kuepusha asizikojolee nguo za Mtume (s.a.w.), Husein (a.s.) akalia, Mtume akasema katika hali ya kama mwenye kukemea, "Tulia ewe Ummul-Fadhli, nguo yangu itafuliwa lakini umemuumiza mwanangu."

Ummul-Fadlili anasema: "Nikamuacha Husein mapajani kwa Mtume na nikasimama kwenda kumletea Mtume (s.a.w.) maji aisafishe nguo yake.

Basi nikaleta maji na nikamkuta Mtume (s.a.w) analia, nikamwambia unalia nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?

Mtume (s.a.w.) akasema: "Hakika Jibril amenijia na kuniambia kwamba Ummati wangu watamuuwa mwanangu huyu basi ole wao, Mwenyezi Mungu asiwafikishie shufaa (maombezi) yangu siku ya Qiyama watu watakaomuuwa."

Al-Imam Husein (a.s.) alipotimiza mwaka mmoja tangu kuzaliwa kwake, walimshukia Mtume (s.a.w.) Malaika kumi na wawili, nyuso zao nyekundu huku wanalia na wakawa wanamuambia Mtume (s.a.w.) kwamba: "Hakika mwanao yatampata masaibu yaIiyompata Habil kutoka kwa Qabil, na kwa ajili hiyo atapewa malipo mema kama alivyopewa Habil, na atakayemuuwa atakuwa na dhambi sawa na dhambi za Qabil.

Hapakubakia Malaika huko Mbinguni ila wote walikuwa wakishuka na kuja kumpa pole na kumuomba awe mvumilivu na pia walikuwa wanamfahamisha malipo atakayolipwa Imam Husein (a.s.), si hivyo tu, bali walikuwa wanamuonyesha udongo wa mahali atakapouawa, na Mtume (s.a.w.) akawa husema: "Ewe Mwenyezi Mungu mpinge atakayempinga na Umlaani atakaye muuwa..."

Alipotimia Imam Husein umri wa miaka miwili Mtume alitoka kufanya safari na katika safari yake hiyo alisimama mahali fulani, basi aliamua kutoendelea na safari yake na mara macho yake yakawa yanabubujika machozi, akaulizwa sababu gani iliyomfanya alie. Mtume (s.a.w.) akasema: "Jibril ananieleza kuhusu ardhi iliyoko kando ya mto Furat iitwayo "KARBALA" mahala ambapo atauawa mwanangu Husein, sasa hivi ni kama nauona uwanja wa mapambano baina yake na adui zake, pia kama kwamba napaona mahala atapozikwa.

Kisha baadaye Bwana Mtume (s.a.w.) aliamua kurudi hali ya kuwa mwenye huzuni na majonzi, akapanda katika Mimbari na akatoa khutba huku Hasan na Husein (a.s.) wakiwa mikononi mwake.

Alipoteremka kwenye Mimbari akaweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa cha Imam Hasan na nikono wa kushoto akauweka kichwani kwa Imam Husein (a.s.) akanyanyua kichwa chake mbinguni akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi Muhammad Mja wako na ni Nabii wako na hawa wawili (Hasan na Husein) ni watu bora katika familia yangu na ni wabora katika kizazi changu na atakuwa mbora mtu atakayewafuata hawa katika Ummati wangu, na hakika Jibril ameniambia kwamba mwanangu huyu atapingwa na atauawa. Ewe Mola mpe baraka nyingi atakapouawa na umfanye awe miongoni mwa Mabwana wa Mashahidi. Ewe Mwenyezi Mungu usimbariki atakayemuuwa na atakayempinga."

Basi baada ya maneno hayo watu wakaangua kilio Msikitini, kisha Mtume akatoa tena khutba nyingine fupi hali yakuwa rangi imembadilika na macho yake yanatoka machozi akasema, "Enyi watu hakika mimi ninawaachia vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Kizazi changu watu wa Nyumba yangu, na hakika viwili hivyo havitatengana mpaka vinifikie katika Haudh, fahamuni kwamba hakika mimi ninavisubiri viwili hivyo, na kwa hakika siwatakeni jambo lolote isipokuwa ni lile aliloniamuru Mola wangu. "Muwapende jamaa zangu". (Kizazi Changu).

Mtume akaendelea kusema: "Fahamuni ya kwamba (siku ya Qiyama) yatanijia makundi matatu katika Ummah huu.

Kundi Ia kwanza litakuwa Ia watu weusi sana, wamezingirwa na Malaika, kisha watasimama mbele yangu nami nitasema: "Ni kina nani nyie"?

"Watashindwa kunitambua, nao watasema: "Sisi ni watu wa Tauhidi mongoni mwa Waarabu.

Basi mimi nitawaambia, "Mimi ndiye Ahmad Nabii wa Waarabu na wasio Waarabu".

Kisha wao watasema: "Sisi ni katika ummati wako".

Nami nitawaambia: "Basi ni vipi mulinifuata katika kizazi changu na katika Kitabu cha Mola Wangu".

Watanijibu: "Ama kitabu tulikipuuza na kizazi chako tulikiangamiza kwa kuwauwa".

Basi nitageuza uso wangu, nao watarudi wakiwa na kiu kali hali ya kuwa nyuso zao ni nyeusi.

Kisha litanijia kundi jingine jeusi mao kuliko lile la mwanzo nami nitawaambia: "Vipi mulinifuata katika vizito viwili, kile kikubwa na kile kidogo, yaani Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu"?

Basi hao watasema: "Ama kile kikubwa (Qur'an) tulikipinga, na ama kile kidogo tulikinyanyasa na kukitawanya ovyo ovyo".

Basi nitawaambia niondokeeni mbele yangu hapo wataondoka hali wakiwa na kiu kali makoo yamewakauka na nyuso zao nyeusi.

Baadaye litanijia kundi jingine Ia watu ambao nyuso zao zinangara kwa nuru.

Basi nami nitawauliza, "Ni kina nani ninyi?"

Watasema: "Sisi ndiyo watu wa neno Ia Tauhidi na Uchamungu, sisi ni Ummati wa Muhammad Mteule, nasi ndiyo bora katika watu wa haki, tulikilinda vema Kitabu cha Mola wetu, tukaihalalisha halali iliyohalalishwa na Kitabu na tukaiharamisha haramu iliyoharamishwa na Kitabu, na tuliwapenda kizazi cha Nabii wetu".

Basi nitawaambia: "Furahini hakika mimi ndiye Nabii wenu Muhammad (s.a.w) na hakika ninyi duniani muliishi kama hivyo mlivyontajia."

Basi hapo nitawanywesha maji kutoka ndani ya Haudhi langu (alilonipa Mwenyezi Mungu) nao watarejea bali ya kuwa kiu imewakatika tena watakuwa na furaha, na baadaye wataingia peponi waishi humo milele na milele.