Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.) ASEMA:

  1. "Ee Allah! Hawa (Ali, Fatima, Hassan na Husain) ndio Ahlul Bait wangu, basi watoharishe kwa tohari kamili."
  2. "Husain anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husain..."
  3. "Hao (Hassan na Husain) Iii maua yangu katika dunia."
  4. "Ewe Mwanangu (Husain)! Mwili wako ni mwili wangu na damu yako ni damu yangu;"
  5. "(Ewe Husain), wewe u Sayyid, mwana wa Sayyid, na ndugu wa Sayyid; wewe u uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu) mwana wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu) na ndugu wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu); na baba wa uthibitisho tisa ambao wa tisa wao ni Qaim wao ambaye atakuwa al-Mahdi."
  6. "Hassan na Husain ni Mashahidi wa Vijana wa Peponi."
  7. "Ewe Mola wangu! Mpende yule ampendae Husain."
  8. "Adhabu atakayoipewa yule mwuaji wa Husain huko Motoni itakuwa sawa na nusu (nzima) ya adhabu yote watakayoipewa wenye dhambi waulimwengu."
  9. "...., Allah hujirafikisha na wale wajirafikishao na Husain yu adui wa wale walio maadui zake."
  10. "Yeyote awapendaye Hassan na Husein amenipenda, na yeyote anayewachukia amenichukia."