 |
Mzuri sana Husaina
Kiitikio
Mzuri sana Husaina Wallahi na kuapia
Giza ilitueneya hapo ulipouliwa
- Ee mwema mwana amani, umekufa kishahidi
Kunusuru hasa dini, ya wetu Mola wadudi
- Umejitolea muhanga, ewe mwana wa Hashima
Ili kuhifadhi mwanga, Nuru kubwa ya Karima
- Kila lote la azizi, kwa Rabuna umetoa
Bila kujali ajizi, hadi kufa kuokoa
- Wanao wenye tohara, Nduguzo waso kifani
Masahaba we imara, umetoa uwanjani
- Kunusuru haki kweli, mfano wako kuiga
Ujabali wenye dhili, kupambana bila woga
- Kuishi na madhalimu, kamwe neema hapana
Ni kudhili jahanamu, maisha hayana maana
|