Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
Husain Akafahamu

Husein akafahamu Ikawa hakuna budi
Mauti yake metimu Dhiki imeshawazidi
Na kweli yake damu Wazee kwa auladi
Adul watachezea Roho zikiteketea

Adui pasi kuchoka Kiu ilo kubwa mno
Waka mwandama mpaka Joto lisilo kifano
Karbala wakafika Vijana wazi midomo
Kusudi wa mwandamia Maji wanahitajia

Furati wakaushika maji wanywayo wanyama
Pasi nafasi kutoka punda, farasi na kima
Mto wakauzunguka Mjukuu wa Hashima
Na maji wakijinywea Adui wakazuja

Kiu ikazidi sana Dhiki ilipo wazidi
Najoto likawabana Akamuona waladi
Imamu na wakewana Asifanye ukaidi
Dhiki ikiwazidia Adui akawendea

Kile kijana swaghiri Kijana kikalalama
Imam wetu Amiri Chembe kimeshika nyama
Tamaa hakuikata Na damu mwili mzima
Ya maji kumpatia Mikononi akafia

Adui wasikubali Mikononi mwa Imamu
Japo lau tone mbili Yote ikajaa damu
Muhali wakaratili Na roho yake ghulamu
Pasi Imani kuingia Ikaiaga dunia

Alipo akikariri Ukazidi ukaidi
Imamu akihubiri Najeshi la mafisadi
Alipata takiswiri Ikawa hapana budi
Chembe wakamrushia Roho zikiangamia

Waliondoka huruma Basi huu ndio mwanzo
Wakawa kama wanyama Wakazidisha mkazo
Pasi kujali dhuluma Pasiwe hata pumbazo
Roho zikiteketea Vitoto vikiumia

 

IMAM HUSAIN (A.S.) ASEMA:

Imam Husain (a.s.) alipokuwa safarini
kwenda Karbala alisema:

"Kama Dini ya (Mtume) Muhammad (sa.w.w.)
haiwezi kuendelea ila kwa kukitoa
mhanga kichwa changu, basi upanga
na uje ukichukue".