Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
Hussein Amefariki

Hakika ni ujahili

Uovu na ukatili

Kuuwa pasi kujali

Bila ya kuzingatia

   

Asikiyae Hakika

Moyo utasikitika

Ma machozi yatatoka

Bila yakufikiria

   

Kwa huyu mtoto wake

Hussein kina chake

Muda kiu imshike

Maji akihitajia

   

Kufika kwa makafiri

Hussein alopojiri

Na mwana huyu saghiri

Maji alimuombea

   

Maadui wasijibu

Kwa kuwazidi ghadhabu

Mmoja wao kajibu

Mshale kuutumia

   

Jibu lake ni mshale

Kumfunma mwana yule

Akafia pale pale

Kifo cha kukusudia

   

Hapo ndipo Hussein

Kwa uchungu wamoyoni

Akaingia vitani

Bila tena kungojea

   

Hussein akapigana

Kishujaa kukazana

Akauwa wengi sana

Kwa nguvu zake jalia

   

Naye mwisho kifo chake

Afanyeje peke yake

Akafa hali yu pweke

Shahidi akajifia

   

Hussein amefariki

Hali yukatika haki

Na hao ni yao dhiki

Walomtenda ubaya