Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
Kwa Mwezi wa Muharram

Naanziliza kauli

Kwa jina lake jalali

Na Swalawati Rasul

Na-ali zake pamoja

   

Mswiba ulo adhimu

Kwa mwezi wa Muharramu

Dhuriya zake Hashimu

Karbala wakingiya

   

Hadithi imetuwambiya

Rasuli ameuswiya

Wapendwa wake dhuriya

Kinyume wakatumiya

   

Umati walibadili

Mahabba yao kwa Ali

Ikawa ni kuwadhili

Na maji kuwaziwiya

   

Yasitoshe walofanya

Ya Mtume kuyakanya

Dhuluma wakamuonya

Vijana kumuuliya

   

Hawakujali hishima

Ya Sayyidati Fatima

Vijana waliye wema

Wa Haidari Aliya

   

Sina budi nitalia

Kukosa kuwatetea

Iwe kwetu mazoweya

Ashura ikingiliya

   

Hadithi walisahau

Mapenzi wakadharau

Wakawauwa na kiu

Furati wakangaliya

   

Walikunwa Kauthari

Maji mema ya fakhari

Pamoja na Answari

Dini waloitetea

   

Yalopita tayakidhi

Kwa Tumwa nipate radhi

Na kwa Mungu ni fawidhi

Na Aya kiisomeya

INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJEUN

Sharif Mohammed Ahmed Al-Huseini
Jomvu Station, Mombasa