 |
SIFA ZA IMAM HASSAN NA IMAM HUSAIN (A.S.)
|
Nawapa na taarifa |
Japo kuwa walikufa |
|
Walikuwa wana sifa |
Njema ilotimilia |
| |
|
|
Walikuwa watukufu |
Tena ni waaminifu |
|
Walo na njema sharafu |
Alowajazi Jalia |
| |
|
|
Walikuwa Maimamu |
Kuongoza Isilamu |
|
Mashujaa walotimu |
Dini kuipigania |
| |
|
|
Walikuwa watu wema |
Vijana wenye heshima |
|
Akiwapenda Hashima |
Wajukuu wa Nabiya |
| |
|
|
Walikuwa wenye dini |
Maovu hawathamini |
|
Na nyingi mno imani |
Nyoyoni ilowangia |
| |
|
|
Walikuwa na huruma |
Isilamu wenye hima |
|
Toka kwa watu wazima |
Na vijana wote pia |
| |
|
|
Walikuwa wasifika |
Duniani kutukuka |
|
Tena waliyoumbia |
Kwa uzuri na tabia |
| |
|
|
Walikuwa makarimu |
Huwezi kuwalaumu |
|
Kisha ni wenye ilimu |
Ya dini na ya dunia |
| |
|
|
Walikuwa wafalume |
Wajukuu wa Mtume |
|
Mashujaa wenye tume |
Vitani kushambulia |
| |
|
|
Sifa zao ni kathiri |
Tena zote ni nzuri |
|
Wala hazina akhiri |
Wallahi zimezidia |
|