 |
Mtoto wake Husseini
|
Jambo jengine ni hili |
La majonzi ikhiwani |
|
Hiki si kisa cha pili |
Ambacho ni cha huzuni |
|
Ni cha kijana rijali |
Mtoto wake Husseini |
| |
|
|
Kadhulumiwa Husseini |
Na wake mwana mchanga |
| |
|
|
Naye kafa madhulumu |
Kijana wa mikononi |
|
Muovu huyo Khasimu |
Adui aso imani |
|
Bure kaimwaga damu |
Ya kijana maskini |
| |
|
|
Kadhulumiwa Husseini |
Na wake mwana mchanga |
| |
|
|
Kifo chake ni dhuluma |
Kijana huyu yakini |
|
Adui aso huruma |
Aso Imani moyoni |
|
Kwa mshale kamfuma |
Ukamwingia mwilini |
| |
|
|
Kadhulumiwa Husseini |
Na wake mwana mchanga |
| |
|
|
Mshale ulimdunga |
Mtoto wake Husseini |
|
Ikawa hapana kinga |
Ya kuiyepuka zani |
|
Akafa mwana mchanga |
Kiumbe cha Rahamani |
| |
|
|
Kadhulumiwa Husseini |
Na wake mwana mchanga |
| |
|
|
Ovu liso wezekana |
Kupata chake kifani |
|
Kiumbe chake rabana |
Kilo safi cha peponi |
|
Walimu-uwa kijana |
Bila kosa asilani |
| |
|
|
Kadhulumiwa Husseini |
Na wake mwana mchanga |
| |
|
|
Huyo ni wake uwele |
Alo mughuri shetani |
|
Alomdunga mshale |
Kipenzi chake amini |
|
Naye piya vile vile |
Ataingia motoni |
| |
|
|
Kadhulumiwa Husseini |
Na wake mwana mchanga |
| |
|
|
Kwa kumuuwa kijana |
Malaika kwa yakini |
|
Hata akatubu sana |
Haipati samahani |
|
Adhabu yake ragana |
Kwake haiwezekani |
| |
|
|
Kadhulumiwa Husseini |
Na wake mwana mchanga |
IMAM HUSAIN (A.S.) ASEMA:
"Kufa kwa heshima ni bora kuliko kuishi kwa aibu".
|