 |
YA SAYYIDNA HUSEINI
|
Kukuomba sina budi |
Ya razaku ya wadudi |
|
Ili utimu mradi |
Yote nalo kusudia |
| |
|
|
Sikutaka kusimama |
Mengi mno kuyasema |
|
Ni mambo kunisukuma |
Ni lazima kuelezea |
| |
|
|
Natokeza hadharani |
Kwa ufupi nibaini |
|
Yalomfika Husseini |
Ya Rabbi niafikia |
| |
|
|
Yale ni mambo adhimu |
Yalomfika Imamu |
|
Sina shaka mwafahamu |
Nami tawahadithia |
| |
|
|
Ule mwaka wa sitini |
Wahijira sikiani |
|
Kaondoka duniani |
Muawiya kajifiya |
| |
|
|
Yazidi alitangaza |
Nchi zote kaeneza |
|
Dini ataiongoza |
Ili watu kumbaiya |
| |
|
|
Barua aliandika |
Madina kaipeleka |
|
Kwa walioikafika |
Nae akimwelezea |
| |
|
|
Kwa makini isomeni |
Mfahamu yalo ndani |
|
Kahitaji kura zenu |
Isilamu wote pia |
| |
|
|
Nazidi kuyabaini |
Yalio mwangu moyoni |
|
Ni kura yake Husseini |
Ufike kumwelezea |
| |
|
|
Husseini kastakimu |
Akasema yakatimu |
|
Huyo ni mtu dhwalimu |
Kidini hakutimiya |
| |
|
|
Kama mimi ni haramu |
Kukubali ya dhwalimu |
|
Sitaki wake msemu |
Mwambiye sitoridhia |
| |
|
|
Kwanza yeye nakiburi |
Ni mlevi hana siri |
|
Kajaa kila fujuri |
Nyote mnamtambua |
| |
|
|
Sitokuwa chini yake |
Hapa na pale afike |
|
Taji hilo silo lake |
Hata yeye yamwelea |
| |
|
|
Mtume alibaini |
Kwa Hassani na Husseini |
|
Ni Maimamu yakini |
Kila mtu kasikia |
| |
|
|
Alifu kumi na mbili |
Barua ziliwasili |
|
Kwa mjukue Rasuli |
Iraq Zilitokea |
| |
|
|
Barua Zilimtaka |
Husseini huko kufika |
|
Ukhalifa kuushika |
Dini kuisimamia |
| |
|
|
Yazidi si mtu mwema |
Sisi sote twafahamia |
|
Na haya tunayosema |
Wewe twakushtakia |
| |
|
|
Husseini hakutwawili |
Katuma lbn Akili |
|
Ili kujua ukweli |
Wa mambo yalomfikiya |
| |
|
|
Alipokewa vizuri |
Wadogo hatakibari |
|
Walimfanya safiri |
Wa Husseini Msifiwa |
| |
|
|
Kisha mambo ligeuka |
Balozi walimwepuka |
|
Mapanga wakayashika |
Muslimu kumuwa |
| |
|
|
Mwezi nane kutimia |
Mfungo tatu sikia |
|
Husseini kashika njia |
Iraqi kaelekea |
| |
|
|
Naswaha zilimfika |
Twakuomba kutotoka |
|
Iraqi usije fika |
Watu wakakukimbia |
| |
|
|
Husseini aliwambiya |
Hayo yote nasikia |
|
Nitakwenda nadhuria |
Mtume kani uswiya |
| |
|
|
Wakiniuwa sijali |
Aliniambiya Rasuli |
|
Kua hayo majangili |
Dhulima watatumia |
| |
|
|
Alipofika njiani |
Ilimaka yakini |
|
Ni hayuko duniani |
Muslim kauwawa |
| |
|
|
Iraq waligeuka |
Unafiki wakashika |
|
Hivi waja kukushika |
Husseini aliambiwa |
| |
|
|
Ule msiba adhimu |
Ulomfika Imamu |
|
Yeye na wake kaumu |
Nakizaziche pamoja |
| |
|
|
Hapa ni pahali gani |
Niambiyeni jamani |
|
Ni Karbala jangwani |
Huseini aliambiwa |
| |
|
|
Ibn Saad Omari |
Najeshile waliswiri |
|
Maudhi na ujeuri |
Imamu wamfanyia |
| |
|
|
Unyama walifanyiwa |
Na kiu iliwauwa |
|
Na maji kuzuiliwa |
Hayo yote watendewa |
| |
|
|
Kauwawa Akbari |
Pia hata Asghari |
|
Na hao watu mashari |
Mungu yuwashuhudia |
| |
|
|
Asghari ni kijana |
Ni mdogo tena sana |
|
Na kiu ilimbana |
Kwa chembe walimuua |
| |
|
|
Husseini aliuuiiza |
Fikirini mukiwaza |
|
Kosa gani tulifanza |
Kutendewa kama haya |
| |
|
|
Himambo yenye huzuni |
Alotendewa Husseini |
|
Nashindwa kuyabaini |
Ukumbuni ngatokea |
| |
|
|
Yangu haki mumetwaa |
Ya ukhalifa sisawa |
|
Na leo mwanisumbua |
Nilipi mwafikiria |
| |
|
|
Au hamkusikia |
Usemi wahashimia |
|
Hapo akiwauswia |
Kuhusu wake dhuria |
| |
|
|
Mama yangu ni Batuli |
Binti yake Rasuli |
|
Na baba yangu ni Ali |
Waswii wake Nabia |
| |
|
|
Ya Husseini walimwaga |
Damu yake bila woga |
|
Walijifanya wajinga |
Ufasiki mewashika |
| |
|
|
Kijukuu cha Rasuli |
Ni Husseini bin Ali |
|
Achinjwa kama ghazali |
Wallahi twakulilia |
| |
|
|
Alipewa kila dhuli |
Mwanao ewe Batuli |
|
Ateswa na majangili |
Waso dini sikiya |
| |
|
|
Walisahau ahadi |
Ya Mtume Muhammadi |
|
Na wote ni mashahidi |
Mtume akiwauswia |
| |
|
|
Alimchinja Husseini |
Bila khofu na huzuni |
|
Na Mungu si Athumani |
Nae atamlipia |
| |
|
|
Ni kifo chenye kutisha |
Tena kina babaisha |
|
Wallahi chahuzunisha |
Kila kinapo tolewa |
| |
|
|
Na Mungu si Athmani |
Twalipa duniani |
|
Wa kesho wenda motoni |
Adhabu yawangojea |
| |
|
|
Hapo ndipo nitafika |
Kalamu chini naweka |
|
Kwa huzuni lonishika |
Siwezi kuendelea |
| |
|
|
Mola atupe Imani |
Yakumpenda Husseini |
|
Tuwe nae na peponi |
Dua zetu zipokea |
| |
|
|
Kisha Swala na Salamu |
Zende hadi kwa Hashimu |
|
Na alize Mainwnu |
Hasidi angachukia |
|