Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

Limetungwa na:
Maallim Abdul Qahari bin Said,
(wa Mtama, Lindi - Tanzania)

UTANGULIZI

Marehemu Maallim Abdul Qahari bin Saidi mwanachuoni mashuhuri wa Madhehebu ya Sunni (Shafii) ndiye aliyeandika shairi hili.

Kwa sauti kubwa na shangwe alilisoma shairi hili katika azimisho Ia Siku ya Imamu Husain (a.s.) iliyofanyika huko Mtama (Lindi, Tanzania) mnamo tarehe mosi Julai mwaka 1961.

Lilirekodiwa katika "Tape Recorder" na kusikilizwa katika miji mingi mingineyo Barani Afrika.

Vile vile liliwahi kuchapishwa mara mbili na "Imamia Mission", ya Lucknow, India.

 

SHAIRI

Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

  1. Bismilah nitajayo, Ni jina la Mola wangu,
    Rahmani isemwavyo, Ya akhera na ulimwengu,
    Rahimi isimuliwavyo, Akhera ya wacha Mungu,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  2. Alhamdu ni sifa za Mola, Lillahi jina Ia Hadhiya,
    Namwalia Rasula, Salaam na neema pia,
    Waalaalihi liula, Zienee kwa wote pia,
    SaIaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  3. Baada ya kumaliza, Sasa natunga shairi,
    Naanza kujituliza, Nitaje kisa na maamuri,
    Kidogo nitatambaza, Si sababu ya kujitafakhari,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  4. Ilahi kamtuma Rasuli, Muhammadi Liamini,
    Awe mtetezi kamili, Aidhihirishe dini,
    Nae kakubali, Kuwa kiongozi wa dini,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein
  5. Kisa ninacho eleza, Maendeleo yaamini,
    Agizo alitimiza, Aliy mtuma Manani,
    Hakuna Ia kumtatiza, Mwislamu moyoni,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  6. Wakati wa maisha yake, Muhamedi Rasuli,
    Alimzaa mtoto mke, Fatumati Libatuli,
    Kamuoza binamiyake, Imamu Sayyidna Ali,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  7. Mola mjuwa falagha, Alli akamzaa Husein
    Mwenyezi Mungu Kawapanga, Wajukuu zake amini,
    Dunia ikawa na mwanga, Wakafurahi Malaika mbinguni,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  8. Siku nyingi zikapita, Mustafa akatawafu,
    Ndipo kuanza matata, Shamu mambo machafu,
    Nakuzitangaza vita, Kuazimu ushupavu,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  9. Dini ikatimiya, Kwa vitendo vya Yazidi,
    Amani zikapotea, Maasi yakazidi,
    Kidogo wafuatao njia, Ya Nabii Muhamadi,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  10. Ikawa nyakati hizo, Zikapunguka imani,
    Ikakithiri michezo, Amani ya Shaitwani,
    Wachache wafuatao nguzo, Nakuthibiti imani,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  11. Na hali hapo zamani, Nabii alitamka,
    Ya Husein minni, Waana ilaika,
    Ndipo kasimama Husein, Naamri akazishika,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  12. Haki ikasimama, Na batili zikaondoka,
    Mpaka siku ya Kiyama, Dini zitabadilika,
    Fahimma hata Fahhama, Uislamu utatajika,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  13. Na kifo chake kwa kamili, Ni fidia ya UisIamu,
    Mfano wa Ismaili, Kwa Nabii Ibrahima,
    Dini leo ni kamili, Imesimama salama,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  14. lmamu alipo sikia, Ilivyo badilika Shamu,
    Aamuruvyo bini Muawiya, Mambo mengi yaharamu,
    Nadini imepotea, Anadai na Uimamu,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  15. Imamu moyo ukasita, Akifikiri tarafa,
    Yazidu anazo zipita Bila ya amali nadhifu,
    Akasema hai hata, Ila nende zangu Kufa,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  16. Tarekhe ishirini na Nane, Akaondoka Madina,
    Kwenda kulitufu Kaaba, Shariya iliyo bayana,
    Yazidi Kakutubu kitaba, Kujisainisha laana,
    Salaam Salaam, lmamu Sayyidna Husein.
  17. Barua ya kutoka Shamu, Ikafika mjini Makka,
    Karifiwa hakimu, Husein muuwe haraka,
    Husein alipofahamu, Ikambidi kuondoka,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  18. Imamu Husein hashirafu, Baada hayo kufahamu,
    Akasema Makka ni tukufu, Kutiya damu haramu,
    Hicho ni kitendo dhaifu, Kakataza Rabi Karimu,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  19. Ikawa tarehe pili, Ya mwezi wa mfunguo nane,
    Karbala akawasili, Kiasi cha saa nane,
    Majeshi ya wakatili, Yakazuia maji wasione,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  20. Mpaka tarehe saba, Mtoni kuna hatari,
    Maadui wameziba, Na maneno ya jeuri,
    Maji na heri kunywa simba, Na nguruwe na makafiri,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  21. Islamu Kataharaki, Kooni kulikauka,
    Kilaakiwalahiki, Maji yao kuwa taka,
    Wao kuzidi hamaki, Huruma imewatoka,
    Salaam Salaam, Imamu Savyidna Husein.
  22. Mama mtoto taabani, Maziwa yamekauka,
    Hamna tone kifuani, Mtoto anahangaika,
    Kayabisika midomoni, Damu zina mdondoka,
    Salaam Salaam, Imamu Sa~yidna Husein.
  23. Wamezuiya hayo maji, Watu elfu tano,
    Wengi mno walindaji, Wa mishale bila mifano,
    Ingawaje anawahitaji, Wala hawana mapatano,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  24. Ikifika siku tatu, Tangu waponyimwa maji
    Wameshikana hao watu, Kwa hali ya uziwiyaji,
    Wakaona hiyana si kitu, Wana nia ya uuwaji,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  25. Tarehe tisa ilipofika, Walitaka waanze vita,
    Imamu Husein aliwataka, Ruhusa ya kuswali wakapata,
    Amuabudu Rabuka, Bila kumfika matata,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  26. Mkuu wa jeshi la Yazidi, Ana moyo mughaladha,
    Omar bini Saadi, Ameajiriwa kwa fedha,
    Akisha timiza ahadi, Hataki kwa Mungu Karadha,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  27. Asubuhi tarehe kumi, Vita ikaumuka,
    Ndipo kuanza uvumi, Mishale kuipachika,
    Omari mtaka dami, Mshale ukamtoka,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  28. Ndiye mwamrishaji, Vita kuamrisha,
    Hakuna tena mkaaji, Muda wao umekwisha,
    Hakuna tena kuhoji hoji, Kawamalizeni maisha,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  29. Ikawa hekaheka, Hali ya vita ni kali,
    Islamu kateseka, Maji yamewawiya mbali,
    Yamradi wana mashaka, Hawanywi wala hawali,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  30. Alipofika mkatili, Mlaanifu mwingi wa balaa,
    Na kisu chake kikali, Yuna kwitwa Shimer,
    Imamu aliomba aswali, Hakupenda amalize swala,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  31. Alipotaka amuuwe, Alitamka Imamu,
    Ebu nikuchungue, Nikujue mjirimu,
    Amuene uso wa Nguruwe, Mara alimfahamu,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  32. Aliambiwa zamani, Uhai wa babu yake,
    Ataye muuwa Husein, Atabadilika sura yake,
    Awe mnyama wa mwituni, Nguruwe kwajina lake,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  33. Ikaja nyingi tufani, Ikatokea kusini,
    Jua likazama mbinguni, Kukawa giza azimu,
    Ikashuka mvua mbinguni, Maji mekundu ya damu
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  34. Wakati walipo mchinja, Adui walifurahi,
    Mwili waliuacha, Ili upondwe na ngamia,
    Na mtoto wakamchinja, Bila ya kumhurumia,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  35. Wanawake wakachojoa, Shungi zao za kichwani,
    Kipita akiwasumbua, Wakatembezwa uriani,
    Kwa ukatili wa kuuwa, Ataulipiza Manani,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  36. Kile kichwa ikabidi, Kama si kichwa cha mtu,
    Kikapelekwa kwa Yazidi, Akakanyage kwa Fimbo,
    Fikara za mkaidi, Si kama fikara za utu,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  37. Yazidi aliona vema, Hajui ameangamia,
    Ndani ya Jahanama, Ndiko aliko ingia,
    Na maji yaja hima, Ndiyo anaumiya,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  38. Hapa ninahitimu, Shairi nimekomesha,
    Ingawaje nina hamu, Yakutaka kuzidisha,
    Rabbi unirehemu, Kwa haya yangu maisha,
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.
  39. Na kila msikiaji, Mwenye roho ya mahaba,
    Rabi mwondolee balaji, Mpokelee kila toba
    Yarabi utufariji, Kwa baraka ya Habiba
    Salaam Salaam, Imamu Sayyidna Husein.

 

MUIENUDDIN CHISHTI AJMERI ASEMA:

Shah ast Husain Badshah ast Husain

Din ast Husain Din Panah ast Husain

Sar dad, Na dad dar daste Yazid

Haqqa ke Binae Iailah ast Husain.

 

Maana yaka:

Husain ni Mfalme (ni Bwana) Husain ni

Mfalme wa Wafalme (ni Bwana wa

Mabwana) Husain ni Dini Husain

ndiye mhifadhi wa Dini.

kichwa alikitoa, bali hakutoa mkono

kuuwake juu ya mkono waYazid.

Hakika Husain ndiye msingi wa

Lailaha iIIaIIah.