Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
Ya Shahida Karbala

  1. Tunasikitika sana kwa kifo chako Husain
    Ewe Husain ya shahida Karbala x 2
  2. Mal-uni alofika kukuua ya Husain
    Na Mungu atayaweka makazi yake motoni
    Ewe Husain ya shahida Karbala x 2
  3. Mbingu zilitikisika kwa kifo chako Husain
    Majabali kupasuka kwa khofu na kwa huzuni
    Ewe Husaini ya shahida Karbala x 2
  4. Upanga uliushika ili kutetea dini
    Kuchezewa yetu dini Husain hukuridhika
    Ewe Husain ya shahida Karbala x 2
  5. Tarehe za tuonyesha kwa kifo chako Husain
    Husain umeondoka umeacha pengo kubwa
    Ewe Husaini ya shahida Karbala x 2
  6. Tunamuomba Manani amiani mal-uni
    Amlani hayawani Yazidi na jeshi lake
    Ewe Husain ya shahida Karbala x 2