Alikuwa miongoni mwa maamiri jeshi wajeshi la Yazid. Yeye alikuwa ni sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye kuhusiana naye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitabiri akisema kuwa atakuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Hivyo basi, mwenye Sharh lbn Abil Hadid, mwenye Ma'arif cha Ibn Qatbiya na mwenye Isti'ab ameelezwa hivi: "Mtume (s.a.w.w.) akiwa anazungumza na Sumrah, Abu Huraira na Hudhaifa bin Yaman alisema kwamba miongoni mwao vule atakayekuwa wa mwisho kufa atakwenda Motoni. Abu Huraira alikuwa kila mara akisema kwamba Hudhaifa alitutangulia kufa na ninategemea kuwa nitakufa kabla ya Sumrah. Hivyo, Sumrah ibn Jundab aliwaishilizia wengine katika kufariki dunia na alikiwepo kwenye mauaji ya Karbala. Imamu Husayn (a.s.) alipoitangaza azma yake ya kwenda Iraq, Samrah alikuwa kwenye jeshi la polisi la Ibn Ziad na alikuwa na desturi ya kuwashawishi watu kwenda kupigana dhidi ya Imamu Husayn (a.s.)." Ingawa aliyatenda yote hayo, kwa sababu tu yu sahaba wa Mtukutu Mtume (s.a.w.w.) amewekwa kwenye kundi la kwanza la wapokeaji wa Ahadithi na mapokezi yake huzipamba Sihah kwenye Isti'ab imeandikwa hivi: "Yeye alikuwa ni sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na wakazihadithia". Hawa watu sita walikuwa ni maamiri-jeshi kwenye majeshi ya Yazid huko Karbala. Sasa tutawataja wale ambao uadui wao kwa Ahlul Bayt (a.s.) kwa ujumla na hasa kwa Imamu Husayn (a.s.) unajidhihirisha wenyewe. Miongoni mwao, wa kwanza wao ni Marwan ibn al-Hakam.
|